LOST ONE OFFICIAL LYRICS

Alivaa sketi inayoangaza ilikuwa nyepesi, 

Fupi unaweza dhani ni kidenti, 

Japo nilikuwa single ila sikuwa mingle alizidisha maringo alipogundua namcheki, 

Haiba ya aibu mfumo wa kibinti, 

Kidogo rangi na lile umbo la kimisi, 

Akiweka pozi nihakiki, 

Alikuwa anang’aa ila ngozi yake ilisanifu dhiki, 

Bado ilikuwa hainiboi kumtazama, 

Macho yangu yalikuwa yana-enjoy alichofanya, 

Kiasili nilikuwa hoi (hoi) kiasi cha kutogundua alikuwa na konvoi la mimama, 

Kwa mtindo wa kujongea kwa madaha

Yule malaika akaanza kusogea nilipokaa, 

Hata kabla sijaamua kumchunguza, 

Macho yaligundua kuwa binti anajiuza, 

Hiyo iliweka ufa moyoni, 

Nilitamani hata kustuka ndotoni, 

Kwakuwa nilipata hisia kali za upendo 

Nikawa tayari hata kujitupa motoni. 

Nilitekwa i only needed her for the rescue, 

That’s how far love can take you, 

Nikataka mpaka kumvika pete 

Awe mchumba  nikasahau mwenzangu anawaza cash tu. 

Ni aina ya wasichana wanaotokea kwenye ndoto, 

Yaani unafumba macho alafu unaona anakulelea watoto, 

Kwa mara ya kwanza maishani mwangu niliwaza ndoa, Hasa baada ya mapenzi ya wasichana wa town kuniboa. 

Akiongozana na kundi la wenzake, 

Akasogea akitoa sauti za kipambe, 

Kila mmoja akijinadi kwa mikogo ya mahaba, 

Nakumbuka mmoja alivua brauzi nimtomase. 

Alijinadi kama ng’ombe mnadani, 

Nikataka nijitose chakani, 

Yaani nijitoe sadaka nilimwona

Ka’ kidani cha dhahabu maisha ya mjini yalifanya ajione hana thamani. 

Tukagonganisha macho kihisia, 

Ndio nikajua nimezama na sijui nitakapoishia, 

Apendae kipofu nikazisahau kasoro 

Nikashuka nikamfungulia mlango akaingia. 

Kwa pupa nikadrive mpaka home, 

Nilipofika hata kuzima gari sikukumbuka, 

Kuna muda nilimkuta uchi kitandani 

Anauliza ka’ tunaenda kavu au kwa ndom. Huh 

Nikamsihi avae nguo, 

Akahamaki akauliza maswali mawili kwa mkupuo, 

Jogoo hawiki braza au ume-mix machaguo, 

Nikamjibu mi msafiri na we’ binti ndo’ kituo. 

Kwa jicho la kufuga kisasi, 

Akanicheki kiasi kwamba niliyumba kinafsi, 

Akanikumbusha hajaja kwangu kutafuta hifadhi, 

Anafanya biashara na kwangu amekuja kikazi

Nikashika usemi uchafu ukiingia kwenye kapu toa

Usitupe kapu kwahiyo sikumwona kama changudoa, 

Nikamwambia nikimwangalia kwanza nawaza kujenga pili familia na tatu ndoa. 

Hakuitikia akanitenga na himaya ya majibu, 

Moyo wake haufunguki na ninahitaji rai, 

Hatukuwa sawa nilitaka kujaribu, akanijibu Kipepeo na nyuki hawatagi yai. 

Akaniruhusu kumkumbatia, 

Akashika mikono yangu akaibusu kwa hisia, 

Sijui alinipa nini nilijikuta naanguka

Kizunguzungu ile kustuka kumekucha. 

Niliamka na mawenge kichwani, 

Nilighafirika kugundua hakwepo chumbani, 

Aliondoka aliniacha na aibu mtaani, 

Maana aliposepa alibeba kila kitu ndani. 

Alikuwa kunguru na nilisahau hafugiki, 

Hata iwe kibudu kwa nyanya na limao haungiki

Alibeba vipi sijui kinachoniuma

Ni kukosa pendo la huyu binti. 

Sitasahau macho yake mawili ya kirembo

Sauti iliyowasilisha upendo, 

Akipigwa vikali na ubatili wa matendo ya mwili wake mzuri ambao haustahili mateso. 

Aliniachia meseji alipoondoka, 

Akinipa pongezi kwamba sikuwa mwoga, kuufuata moyo wangu akaniomba msamaha akisema hawezi kuenzi penzi ambalo kwa wazazi alikosa. 

Sawa ah! Nimekusamehe zamani mami, 

Pendo lako dawa ewe baniani, 

Niahidi utawasamehe wazazi wako pia

Ambao wamefanya uonekane shetani honey.  Yeah

I’m kinda lost I do things i ain’t suppose to

I thought you’ll be my best friend that I can talk to, 

I wanna change if you wanna change I’ll support you

I think we both need the way out that we can walk through. 

Ah popote ulipo ambapo info inafika, 

Bado mrume nipo miaka inapita nauandika huu wimbo umenifundisha nisitue mzigo kama ninahisi sijafika. 

Naoa kesho na nina hamu kukukuta

Nikwambie dunia safi binadamu ndo’ uchafuka, 

Ni kawaida usisahau kutabasamu kukikucha, 

Nakuombea afya kwenye nyama damu na mifupa. 

Ah!! 

Pellentesque tellus 

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing eli.

Phasellus luctus

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing eli.

Etiam sodales

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing eli.

Nullam eu sem

responsive design

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

super features

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

drag and drop

HATIA OFFICIAL LYRICS

[Ah.!
Niambie ilianza vipi najua haikuanza ghafla
Zipi dalili maana hata mafua huanza na chafya
Kivipi mi kaka’ako na ulisita kuniambia ukafanya siri ina maana kimsingi nawe ulitaka

Ah! Kimsingi nawe ulitaka kumbuka
Tangu baba mzee Muggo anakufa
Alituusia uaminifu na ndio nguzo uliyoiangusha
Nashangaa bado nafsi yako hijasuta

Maana bado natamani kukujali
Mdogo wangu natamani sana lakini imani yangu imekufa tayari
Sometimes nakwenda mbali
Natamani kukudhuru busara inaniweka huru nagundua mi sio mshari

Ulianza vipi kumtamani wife Je ni siku namwoa?
Au ulianza kabla ya siku ya ndoa
Na ndio maana siku ya harusi ushirikiano ilikuwa ni ishu kutoa
Kama harusi ni pingu nang’oa

Sihitaji tena
Najiuliza kwanini nilibashiri
Lakini nikapuuzia dalili
Kwanini nili….. Ah
It all makes sense now

Subiri mwanaizaya subiri it all makes sense now
Mwezi wa pili hanipi penzi now
Yaani kipindi nashusha pensi down
Ananiambia kuwa amechoka anahisi kama homa hawezi… How??

(nimiminie wisky)
Sikujua kuwaacha pamoja home ilikuwa ni risky
That’s why I’ve been away for so long and she never missed me

Sikiza…
Sijui unachofikiri rohoni bado
Maana upo kimya niseme huoni mwisho huoni mwanzo
Ulikataa kusoma chuoni ng’ambo
Ubaki ule ninapokula kweli kikulacho ki nguoni mwako

Tulisimama kama mdogo na kaka umeng’oa nguzo
Hongera kwakuwa Mpumbavu yanipasa kutoa tuzo
Have you started using cannabis??
Man i thought we are brothers
I thought we are bond now we are enemies
Enemies…

Hii maradufu imeniumiza
Acha uliponiangushia mninga
Au ulipogusa mzinga nikakuokoa
Upole ulizidi ukaniona mjinga
Ukaamua kumshika sharubu simba

Ah! Remember we use to build a snowman
Go school together playing ball and
I can’t believe that my own brother sheg my own wife on my own bed
( On my own bed..)

Nilitaka tuwe saresare
Ningaefadhiri mbuzi ningekuacha uwe palepale
Mabinti hawaishi ukianza huwamalizi ukasahau visima vingi ila maji ni yaleyale

Tulikuwa kama mwiko na wali
Ulikuwa kijana mzuri mdogo nakuvusha kijito cha maji
Umebadilika umepoteza nguvu na ufanisi
Mtaa mzima unatembeza rungu kama mlinzi

Nilijitoa sadaka ili ufike far
Maana sikutaka ikufike njaa
Hukutaka unisikilize na
Ukachagua kuvunja moyo wangu vipande i don’t even know where the other pieces are

Vile Niliamua kukulea
Ah nikakulea kama yai kama…
Ukaamua kunionea

Kaa kimya.. Kaa kimya ngoja nibonge
We ni mdogo wangu toka nitoke
Inaniumiza sikukwambia tangu mwanzo kwamba huu mwaka wa tatu mi na wife…
Tunagonga vidonge

Oh men she killed you
That devil killed you
Labda nimeekuua mwenyewe labda ningekuambia kuwa.. Kuwa sisi ni waathirika ila nikasita….
Men I’m still a fool

Yes I’m still a fool..

Nikiandika overall summary
Nimekuwa mjinga ’cause i killed my own family

(Nimekuwa mjinga ’cause I killed my own family…)

Kwakuwa nimekulea nimewajibika
Umesoma umepata kazi ya kuheshimika
Nahisi kama kazi yangu imekwisha nimemaliza, naondoka naenda mbali maana kuwaona inaniumiza

Zingatieni tiba…

(Zingatieni tiba…)

(Zingatieni tiba….

(Zingatieni tiba….)

Kumbuka kuugua sio kufa.. Niahidi hautajuta..

Kwaheri

)

Kumbuka kuugua sio kufa.. Niahidi hautajuta..

Kwaheri

HATIA II OFFICIAL LYRICS

[Ah!
Nilipaa sasa natua
Kwenye/kwenye
Siri ya moyo
Na siri ya moyo
Anayeijua mwenye/
Mwenye ujasiri wa
Kutunza nafanya
Ninachodhani ni
Sahihi kitachotokea
Nitajua mbele

Wanasema mwanaharamu
Haijui laana/ kashalaanika
Nasikitika kuwa haujui
Kama/ naonekana ka’
Kondoo kwa mchungaji
Lakini…lakini kwa ndani
Mi’ ni chui mama

Kwa mfano nakuita mpenzi/
Na tabasamu zuri wakati
Najua kuwa sikupendi/
Kuitoa hii siri ndo’ siwezi/
Kwahiyo nitakudanganya
Mpaka ifike siku niutimize
Ushenzi

Huwa nawaza nikuweke
Ufahamu/ mtambue
Kuwa mpo wengi
Na lengo niwateke
Kwa zamu/ niwaumize
Ili mpeleke salamu/
Masikini mrembo
Nashangaa jinsi unavo’ngoja
Pete kwa hamu

Vile hunioni kwenye
Makundi ya baa/
Na bahati nzuri haujawahi
Kusikia nikizushiwa uzushi
Kitaa/ nakununulia
Rubi kadhaa/ unahisi nakujali
Kumbe unampigia mbuzi gitaa

Sometimes unanisongea nguna/
Au wali ukidhani mi’ najali ilihali
Sina habari, sina hisia siwazi
Hata kukuonea huruma/
Na sibadili dhambi hata
Mbingu ikisogea nyuma

Ah!
Nashiriki  nawe nyakati
Twitter mpaka instagram/
Picha unani-hashtag drunk in love/
Nanunua brand za gharama za
Hand bag/ perfume kali
Simu ya ghali breakfast
Zanzibar/

Haimaanishi kuwa
Tunaianza safari/
Nataka nikuandalie maumivu
Makali/ nahitaji nikuguse
Ili kila unachokiona
Kiwe kinafanya unikumbuke
Ni hatari

Inaitwa zuia nanga kabla
Bado haijang’oa/
Maana haujaheshimu
Mvua kama bado hujaloa/
Kwa huu mchango ninaotoa/
Ndo’ unafanya unazama
Zaidi kiasi unaiwaza mipango
Ya ndoa

Jicho la tatu hauna
Fungua jicho lako la pili/
Utagundua kila ninachofanya
Kwako batili/ unanipenda mno
Ndo’ maana haujaona bado
Dalili/ kuwa we sio wa kwanza
Wala haupo kwenye
Mpango wa pili
Ah!!

Unaniletea zawadi toka
Majuu/ kuna wenzio
Nilishawaacha
Na walinichora tattoo/
Mi sio tunda mama…
Mama mi’ kidonda
Utachelewa kusonga
Ka’ bado unaingoja nafuu

Sherehe ya birthday yako
Kwenye ‘temple’ ya anasa/
Umekuwa ‘mental’ kwa
Huu mwendo ndo’
Umenasa/
Kiasi unahisi huu ni upendo
Na sasa/ hautambui kuwa
Tukishiriki tendo tu nakuacha

Kichwa changu hichi,kichwa
Changu kishajadili/ kwamba
Nitalala na wewe na
Wewe na haifiki jumapili/
Nitakuwa nimeshakuacha
Ah! utanitafuta
Kwenye simu ambayo
Namba nitakuwa nishaibadili

Utanitafuta mara mbili/
Mara tatu kisha nne
Utagundua kurudi
Sina dalili/ ngoja ngoja
Itang’ata moyo wako
Kikatili/ mja wa
Watu maumivu
Hukujiandaa kuyakabili

Utanipamba majina ya
Kikafili/ sitasikia maana
Nitakuwa mbali nishasafiri/
Nishasahau utatunga nahau
Kukanda mwili/ na huo
Wakati haukuwahi kuutabiri/
Ila upo

Utaumia utashindwa kusimulia/
Utaniulizia kwa wanaonijua
Watakwambia/ kwamba
Hauna tena chako
Okota vipande vya moyo wako
Nenda zako kaandike
Tanzia

Kisha watajua wenzio/
Wanafiki watacheka
Wanaokujali wataangua kilio/
Watakusindikiza kulia/
Watakupa pole wengine watasema
Tulikuambia/ kuwa
Wanaume wote mbwa!!

Taswira itazongwa
Na wingu/
Picha utazichoma
Kwa kisu/
Utanitukana mara mwana
Haramu mara malaya/
Rafiki zako wakuu watakuwa
Filamu na riwaya

Wimbo niliokuimbia
Kamwe hautokukonga/
Utachoma mkuki moyoni
Kisha kunyonga/
Utaendelea kungoja/
Utagundua mvumilivu
Hali mbivu hiyo
Methali iliongopa/
Utagundua ilikuwa
Ni soga/

Hii itafanya ukonde
Na kuanza/
Kutumia pombe na ganja/
Nayajua haya yote
Kwa maana ndo nilikotoka/
Utasimama kijasiri
Na mwisho utadondoka/
‘sikiliza’

Wataleta daktari
Akuulize nini shida/
Hawatapata
Jawabu kabisa/
Wataleta sheikh
Wataleta mchungaji
Wa kanisa/
Watasahau kwamba
Moyo uliovunjika
Hauna tiba

Natamani nikuambie kuwa nimekuteka makusudi/
Maana unasikia na hujifunzi/
Nikuumize kama mke wangu mpuuzi/  aliyekimbia na rafiki yangu siku moja baada ya harusi

Nilishaambiwa na
Mama nikapuuzia/
Kuwa haujawahi
Kupenda kama
Haujawahi kulia/
Kuna muda mtu mbaya
Hutengwa na hatia/
Maana kafiri hazaliwi
Utengenezwa na dunia

Ukijiua sitakuona
Mzembe amini/
Nitakuvalisha pete
Ruksa uipeleke baharini/
Najua tiba ya
Upweke amini/
Mwisho wako ni
Kuwa kicheche kama
Mimi

Hapo utajua kunihukumu
Sio haki/
Mwanamke kama
Wewe ndio amenifanya
Niwe muasi/
Bila hofu wala
Kiwewe/
Nitaendelea kuzunguka
Kutafuta wasichana
Vipofu kama wewe

Sina hatia ..

KANISA OFFICIAL LYRICS

Yoh!
Salamu kanisa wako mpendwa katika bwana,katika wana waliotaka kufeli nami nazama, 
tangu jana uwepo wako haupingiki,kisa una nguvu ya kuwavuta wasiosadiki
Sikuhitaji mambo ya kugawana madhehebu,waumini dhaifu wanahama hama kama wehu,ikiwa tangu kale wazazi wangu walichanganywa,basi hakika sitahukumiwa kwa kudanganywa, (kanisa)
Sidhani ka’ upo sawa kunibeza,maana hata wewe unapitisha dawa za kulevya,tukianza ku-confess yaliyo nyuma ya pazia,we utachomwa moto alafu mi nitaachwa nakuapia
Sitaki kuamini kuwa sadaka au kusifu kwa fasihi, ndio vitanipeleka kwa masihi,kitachonionyesha mbingu ni bidii,ya kutenda mema so sitaki kujua dini ipi ni sahihi, ah!
Kanisa unatudanganya kirahisi,nyumba ya mungu ni mioyo yetu nahakiki,kwakuwa saa hizi, jua kali njaa hizizinafanya ukubali kugeuka taasisi
Usinishushe hadhi nikizini,ikiwa unafuga wachungaji wenye dhambi kama mimi,kanisa nakupa pole,nje msafi ndani mchafu naomba tusinyoosheane vidole
Kanisa unaniasa,niache kutamani vyeo na wewe unajihusisha na siasa,kama mji wa sodoma ulizikwa na anasa,mwisho wako upo kama hautabadilika sasa
Haufanani na meli ya nuhu,unaniomba mchango na kodi nimefeli kumudu,kanisa unanitapeli kizungu,unanizungusha haunionyeshi kanisa la kweli la mungu
Eti manabii wana vyeti, 
kanisa lina account ya mitandao ya kijamii mpaka benki,wahubiri wanavutana kinguvu,kanisa unajitangaza kutafuta umaarufu?
Unapishana na muda hakika,unachojua pekee we ni kufa kuzika,unanishauri nije kwako ndoa ikiyumba kanisa,kichekesho kwamba wewe ndio umeyumba kabisa ah!!
Kanisa nilikuja uniongoze, 
nimpende mungu wewe unaifunza nimwogope, 
jua kali lilinifunza kukabanikakupa maisha na cha ajabu haujanifunza chochote
Nasikia una pande mbili za sarafu,upande mzuri na upande unaoingia dili mpaka na wafu,na unanifundisha baya haliwi na thawabu,nilikuwa mjinga na sasa nayabashiri majawabu
Tunahitaji mafunzo halisia,wakati mbinu zako zimejaa mafumbo na sheria,kanisa tunaishi na wanafki kudadeki,unajifanya rafiki sababu ya ulafi wa chenchi
Ikiwa huruma ya jah haina kipimo,basi kati ya wanaoomba msamaha nami nimo,dhambi zako sawa? Tumezidiana kimo, 
mungu aliye hai akuepushie shimo, kanisa huh!
Umeshindwa kukidhi,utu unakutoka sababu umeshikwa na dhiki,unasahau lengo unasahau umesimamishwa na sisi,pesa inakuyumbisha nawe unayumbisha misingi
Kijiwe chako hakikuniingia akilini,nikafata vijiwe vya pombe vikanitia umasikini,kisa kila aliyenionyesha nia nilimuamini,leo siwaoni wote wameingia mitini
Haupo hata kwenye hadhi ya utatu,mungu baba, mwana, roho kisa kazi za uchafu,kanisa hauchezi Pasi ni rafu, 
unaremba altale kuliko hata nafsi za watu
Kwa sasa ninahisi una bifu, na taasisi binafsi kwa sababu haukuwa mwangalifu,kama ndani yako wanaoishi wadanganyifu,na wanasali hautazalisha watakatifu
Kuwa mkweli ni wapi ulipoishindwa nielewe,hiyo siri yako hauwezi ukaificha milele,kama nitachomwa moto wa kukushika ni wewe,nishakusafisha kuliko kujisafisha mwenyewe aah!!

NDOANO OFFICIAL LYRICS

Okay

Ah
Chukua kitabu fungua page sixty three
Tusome hii part ya love and its mystery
Haiwezi elezwa kwa science, math labda history
Inaitwa ndoa ni half loss half victory

Kauli ya kwamba sikuachi mpaka kifo ni kama sifa
Inasemwa na wengi ila wachache wanamaanisha
Wale wapambe na mashahidi wa kujivika
Au keki na maua ambayo mwisho hupukutika ni….

Nini maana ya suti shela au rangi ya bazee?
Nini maana ya vile vikao kadi tarehe?
Nini maana ya maandalizi hadi sherehe?
Nini maana ya kiapo kwa padri na sheikh?

Imeandikwa

“kila penye watu lipo la kujifunza”
Tembea uone kukaa ndani ni kujifunga
Kama wanandoa si binadamu wanaofugwa
Kwanini iwekwe ahadi isiyoweza kutunzwa?
Ndoa ni…….?

(mchagizaji) NDOANO

Ndoa ni ile iliyoandikwa na sheria au dini?
Au shuruti baada ya hatia ya kuzini?
Ni jukumu unalovishwa baada ya ugoni?
Au bashasha unalojivika usoni

Watu wajue umeridhia, makubaliano na riba za njaa
Ahadi ya kuwa pamoja kwenye shida na raha
Ahadi inayovunjwa ka’ sheria inavyopindwa na jamaa
Ndoa si akiba ni sanaa
Ndoa ni…..

Sanaa ya kukaa nafasi ya mwenzi
Sanaa ya kusahau maudhi na kuzikumbuka tenzi
Za msamaha au kuzuga kujutia kitendo
Sanaa ya kuzuga kubadili mwenendo
Ndoa ni……

Ule umoja mfano wa timu
Kwenye mechi wanaomba mapumziko
Ndoa inafungwa na sala na toba za mizimu
Lakini inavunjika kwa meseji moja tu ya simu
Ndoa ni……

Hakuna kitu halisi kwenye ndoa labda huyo mtoto
Ni idadi ya vipande baada ya kuvunja vyombo
Ndoa si pete zinazozonga mikono
Ndoa ni upendo unaobakia baada ya kuchoka kingono
Ndoa ni…

Ni ka’ kikundi cha masela
Wanaodhani kuwa wamekua
Ndoa ni kuvumilia maudhi yanayokera
Ndoa ni maigizo yasiyo na hela ndoa ni jela
Ndoa ni….

Kuzijua kelele
Kutambua shangwe na vigeregere
Ambacho hautajua milele
Unapodondosha chozi kwa mchezo uliouchagua mwenyewe

Ndoa si…..kwa ajili yako ni kwa ajili ya watoto
Kuweka ndoto kando na kuzivaa changamoto
Ndoa ni kukumbatia kaa la moto
Ndoa ni jua kali ndoa ni joto
Ndoa ni….

(mchagizaji) NDOANO

Ah
Asiyejua ni nani?
Kuwa mlioana msikitini na mkaachana mahakamani
Kwa kuwa ndoa si nyepesi ndoa ni yai
Ndoa ni kama kesi ya jinai, ndoa ni…

Ndoa ni hukumu wanasema
Ndoa ni ngumu jamani, ndoa ni sumu
Au mpaka mume alete….UKIMWI nyumbani
Ndio uamini kuwa ndoa si tunu

Ndoa ni maisha baada ya harusi
Ile sherehe uliyoiota ndotoni
Ndoa si drama mbele ya watu nyomi
Ndoa ya kweli huanzia moyoni

Ndoa ni….FUMBO

Our Core CollectionWALL PHOTO FOR 30,000 TZS

WALL PHOTO, WOODEN AND SHINY. SIZED A3