NDOANO OFFICIAL LYRICS

Okay

Ah
Chukua kitabu fungua page sixty three
Tusome hii part ya love and its mystery
Haiwezi elezwa kwa science, math labda history
Inaitwa ndoa ni half loss half victory

Kauli ya kwamba sikuachi mpaka kifo ni kama sifa
Inasemwa na wengi ila wachache wanamaanisha
Wale wapambe na mashahidi wa kujivika
Au keki na maua ambayo mwisho hupukutika ni….

Nini maana ya suti shela au rangi ya bazee?
Nini maana ya vile vikao kadi tarehe?
Nini maana ya maandalizi hadi sherehe?
Nini maana ya kiapo kwa padri na sheikh?

Imeandikwa

“kila penye watu lipo la kujifunza”
Tembea uone kukaa ndani ni kujifunga
Kama wanandoa si binadamu wanaofugwa
Kwanini iwekwe ahadi isiyoweza kutunzwa?
Ndoa ni…….?

(mchagizaji) NDOANO

Ndoa ni ile iliyoandikwa na sheria au dini?
Au shuruti baada ya hatia ya kuzini?
Ni jukumu unalovishwa baada ya ugoni?
Au bashasha unalojivika usoni

Watu wajue umeridhia, makubaliano na riba za njaa
Ahadi ya kuwa pamoja kwenye shida na raha
Ahadi inayovunjwa ka’ sheria inavyopindwa na jamaa
Ndoa si akiba ni sanaa
Ndoa ni…..

Sanaa ya kukaa nafasi ya mwenzi
Sanaa ya kusahau maudhi na kuzikumbuka tenzi
Za msamaha au kuzuga kujutia kitendo
Sanaa ya kuzuga kubadili mwenendo
Ndoa ni……

Ule umoja mfano wa timu
Kwenye mechi wanaomba mapumziko
Ndoa inafungwa na sala na toba za mizimu
Lakini inavunjika kwa meseji moja tu ya simu
Ndoa ni……

Hakuna kitu halisi kwenye ndoa labda huyo mtoto
Ni idadi ya vipande baada ya kuvunja vyombo
Ndoa si pete zinazozonga mikono
Ndoa ni upendo unaobakia baada ya kuchoka kingono
Ndoa ni…

Ni ka’ kikundi cha masela
Wanaodhani kuwa wamekua
Ndoa ni kuvumilia maudhi yanayokera
Ndoa ni maigizo yasiyo na hela ndoa ni jela
Ndoa ni….

Kuzijua kelele
Kutambua shangwe na vigeregere
Ambacho hautajua milele
Unapodondosha chozi kwa mchezo uliouchagua mwenyewe

Ndoa si…..kwa ajili yako ni kwa ajili ya watoto
Kuweka ndoto kando na kuzivaa changamoto
Ndoa ni kukumbatia kaa la moto
Ndoa ni jua kali ndoa ni joto
Ndoa ni….

(mchagizaji) NDOANO

Ah
Asiyejua ni nani?
Kuwa mlioana msikitini na mkaachana mahakamani
Kwa kuwa ndoa si nyepesi ndoa ni yai
Ndoa ni kama kesi ya jinai, ndoa ni…

Ndoa ni hukumu wanasema
Ndoa ni ngumu jamani, ndoa ni sumu
Au mpaka mume alete….UKIMWI nyumbani
Ndio uamini kuwa ndoa si tunu

Ndoa ni maisha baada ya harusi
Ile sherehe uliyoiota ndotoni
Ndoa si drama mbele ya watu nyomi
Ndoa ya kweli huanzia moyoni

Ndoa ni….FUMBO

Leave a Reply

Your email address will not be published.