Mwaka 2024 unaelekea ukingoni, Kwa hitaji la wengi nimeandaa list yenye baadhi ya  Albums nilizosikiliza, vitabu nilivyosoma, makala nilizosoma na filamu nilizoangalia kwa mwaka huu wote.

VITABU

Mwaka huu nilisoma vitabu vitatu na hii ndio review yangu kwa ufupi kwa kila kimoja.

1. Ujamaa - Essay on Socialism - The late Julius K. Nyerere

Kitabu kilichapichwa kwa mara ya kwanza mwaka 1961, na kufanyiwa marejeo mara kadhaa na baadaye kutafsiriwa kwa lugha ya kiingereza mwaka 1968. Nilikisoma kwa mara ya kwanza mwaka 2013 lakini nikawiwa kurudia sasa nikiamini kuwa na uwezo wa kuelewa maudhui yake kwa mapana yake. Kwenye nakala hii mwandishi anajadili maono ya hayati Baba wa taifa Julius Kambarage Nyerere kuhusu wazo lake la kuwepo kwa aina maalumu ya ujamaa inayoendana kwa asilimia mia moja na tamaduni, mira na desturi, aina ya itikadi, kiwango cha uelimikaji na mtindo wa maisha wa nchi za kiafirka (Specifically Tanzania). Wazo la aina hii ya ujamaa lilitumika kama sera kuu ya chama cha siasa cha TANU ambacho Mwalimu alikuwa ni mwenyekiti wake. Mwandishi alielezea mafanikio na changamoto ya wazo hili hasa kwenye practicability and implimitations. Nakala hii ilibaki kumbukumbu ya juhudi za mwanzo za kumkomboa mwananchi masikini baada ya Ukoloni. Hili andiko lilisanifisha kanuni muhimu zilizosimamia haki na usawa kama zilivyojadiliwa kwenye azimio la Arusha. Nukuu yangu pendwa kutoka kwenye nakala hii ni ile iliyomnukuu mwalimu kuhusu umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii kwa ustawi wa familia zetu, akisema "‘Mgeni siku mbili; siku ya tatu mpe jembe’

2. The moral Lanscape - How science can determine human values - Sam Harris

Binadamu wa karne ya 21 wamekuwa kama kitu kimoja kwa sababu ya kukua kwa teknolojia hasa kwenye eneo la mawasiliano na usafirishaji. kukua huku kumefanya dunia kuwa ndogo. Binadamu wanajijamiisha kwa karibu na kwa haraka zaidi bila kujali maeneo waliopo. Hii imekuza umuhimu wa mazungumzo kuhusu falsafa ya maadili. Mwandishi wa The Moral Landscape, Kitabu kilichochapishwa mwaka 2010, Sam Harris anajadili wazo la kuhusianisha maadili na ustawi wa maisha ya binadamu (Well-being) akisema Mijadala ya maadili haitakuwa na maana kama haitahusisha ustawi wa maisha ya binadamu na wanyama. Pia alijadili kwa kiasi gani sayansi itaweza kutupa kweli ya nini maana ya ustawi hasa kwenye eneo la afya ya akili, mwili na hisia za binadamu. Pia alijadili tamaduni na imani mbalimbali zinavyoweza kuhatarisha afya ya mwili, akili na hisia, lakini pia afya ya uchumi wa binadamu. Nukuu yangu pendwa kutoka kwenye kitabu hiki ni "Wanawake na wanaume walio kwenye hukumu za kunyongwa, wapo pale kwa sababu ya mchanganyiko wa malezi mabaya, mawazo na itikadi mbaya, imani mbaya, vinasaba mbaya au bahati mbaya"

3. Who we wrestle with God - Jordan Peterson

Kitabu hiki kilichapishwa November 2024, Ndio kilikuwa kitabu cha mwisho kusoma mwaka huu. Mwandishi anajadili hadithi za mwanzo kabisa za kifasihi na umuhimu wake kwenye maisha ya sasa. Mwandishi anaamini kuwa fasihi za zamani ni muhimu kwa sababu zinatupa picha ya mtindo wa kufikiri wa jamii za kale (their thinking process). Mwandishi pia anajadili dhana ya ukaidi, sadaka, mateso na ushindi kwa kutumia hadithi mbalimbali za kibiblia. Jordan anachagua Biblia kuelezea subject matters zake akiamini ni kitabu stahiki zaidi kiushawishi, kiumri na kiuhalisia (authenticity). Moja ya subject matter alizojadili mwandishi ni IMANI na kujitoa SADAKA (Faith and sacrifice). Anasema dunia na mapana ni kubwa sana kiasi hatuwezi kuimaliza kuielewa hivyo kwenye maisha mafupi ya binadamu huwa tunachagua vile tunaavyoona ni muhimu. Na hapo ndio Imani na sadaka vinapokuja kwani kuchagua ni kuamini kuwa upo sawa na machaguo yako na unatoa sadaka vingine vyote ili kufuata unachoona ni sahihi (cost of choices/opportunity). Mfano wa hadithi alizotumia kujadili maudhui ni ile hadithi ya Yona aliyeikimbia sauti ya Mungu iliyomtuma kwenda Nineveh kueneza habari njema, Yona alikaidi na mwishowe kumezwa na samaki. Mwandishi alihusisha hii hadithi na athari za kukimbia majukumu kwa nafasi uliyopewa. Nukuu yangu pendwa kwenye kitabu hiki ni "kanuni mbaya zikienziwa, wafalme wabaya wakisimamishwa na maadili mabaya yakiwekwa na watu, ni watu wenyewe ndio wataangamia"

FILAMU

Nilipata wasaa wa kuangalia filamu kadhaa mwaka 2024 na hizi ni 5 zilizonivutia zaidi.

1. 12 angry men ya mwaka 1957

Filamu inahusu baraza la waamuzi 12 waliopewa jukumu na mamlaka ya kuamua kesi ya kijana aliyetuhumiwa kumuua mzazi wake. Kesi iliyoonekana ni ya dakika kadhaa tu kwa sababu ya nguvu ya ushahidi uliowekwa ila inageuka kuwa shughuli ya kichunguzi. Waamuzi 11 waliamini kuwa mtuhumiwa ni mkosefu na anastahili adhabu wakati mmoja akiwa na shaka na aina ya ushahidi ulioletwa, hivyo akachukua jukumu kuwashawishi waamuzi wenzake kujadili upya ushahidi ili kuondoa shaka. Filamu ya seti moja ila ilikuwa na uwezo wa kubakisha shauku muda wote kwa sababu ya ubora wa mazungumzo na story progression. Moja ya nukuu niliyoipenda kwenye Filamu hii ni "Kama unataka kupiga kura kuwa fulani ana hatia, sema kwa sababu una uhakika ana hatia na sio kwa sababu umechoka kusikiliza shauri". Mtoa nukuu alikuwa anajaribu kuwaambia waamuzi wengine kuwa wasitoe maamuzi wa sababu wamechoka na wanataka kwenda nyumbani

2. Schindller's list -1993

Filamu ya wasifu wa kweli (Autobiography) inayomuhusu Oskar Schindler, Mfanyabiashara mwenye tamaa ya pesa aliyeingiwa na ubinadamu kiasi kugeuza kiwanda chake kuwa kimbilio la wayahudi waliothiriwa na serikali ya ki-nazi ya Ujerumani. Filamu hii iliandaliwa kuenzi mchango wa Oskar kwenye mapambano dhidi ya ukatili wa serikali ile chini ya Adolf Hitler. Moja ya nukuu muhimu niliyoipenda kwenye Filamu hii ni "Nguvu ni pale ukiwa na kila sababu ya kuua alafu hauui" akijadili umuhimu wa kusamehe na moja ya wafanyakazi wa serikali ya kibazazi ya ujerumani.

3. Enemy - 2013

Filamu ya kisaikolojia inayomuhusu mhadhiri wa chuo kikuu anayemuona mtu anayefanana naye kwa asilimia 100 kwa mara ya kwanza baada ya kuambiwa na rafiki yake kuwa wamefanana. Anaenda kuangalia filamu zake baada ya kugundua ni mwigizaji. Kiu ya kumchunguza inaishia kumuweka kwenye njiapanda inayozaa matatizo makubwa. Mhadhiri huyu analea mazoea yake ya kuchunguza familia ya mtu huyu na mwishowe kuingia matatani. Filamu inayojadili umuhimu wa kurekebisha mazoea mabaya kabla hayajawa tabia. Mazoea kwenye filamu yanawakilishwa na buibui mdogo anayeonyeshwa mwanzo wa filamu kisha kuwa mkubwa mwisho wa filamu.

4. The Assasionation of JESSE JAMES by the Coward ROBERT FORD - 2007

Mja mwoga Robert Ford anategemea kulakiwa kishujaa na jamii yake baada ya kumuua jambazi anayeogopwa kwenye mji wake. Kiu ya umaarufu na heshima inamfanya kubadili jina kisha kuandika kitabu kusheherekea mauaji yake mwenyewe lakini bado jambazi Jesse anaimbwa kama shujaa huku yeye akiwa hatambuliki kabisa. Hasira inampanda baada ya filamu kutengenezwa kumuenzi Jesse. Robert anajaribu kuishi na uhalisia kuwa watu hawamwoni kama shujaa bila mafanikio, Kiu yake ya kuheshimiwa inarudi na mwishowe inamwingiza kwenye kifo.

5. Cosmos: A Spacetime Odyssey, Season 1
Msimu wa kwanza wa mfululizo wa sukununu ya binadamu kuhusu ulimwengu na elimu ya anga. Chaneli ya National Geographic wanaungana na Mkufunzi wa masuala ya astrofizikia Neil de Grease Tyson kubadili kitabu kuwa onyesho la televisheni.

ALBUMS

Nilisikiza album kadhaa kwa minajiri ya burudani na elimu na hizi ndio zilinivutia zaidi. 

1. The auditorium Vol 1 by Common & Pete Rock
2. Knock Madness by Marcus Hopsin
3. Mapinduzi halisi by Professor Jay
4. Extiction level Event 1 by Busta Rhymes
5. Extiction level Event 2 by Busta Rhymes
6. Mhadhiri by Maalim Nash
7. Mitaa flani by Songa
8. In my room by Jacob Collier
9. Dawn by Yebba

156 comments

  1. Mapinduzi Halisi ni moja ya kanda mseto bora ya muda wote katika historia ya muziki wa Tanzania.

    ReplyDelete
  2. πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™

    ReplyDelete
  3. πŸ’―πŸ’―πŸ’―

    ReplyDelete
  4. No wonder, you are Disaster

    ReplyDelete
  5. The black marradona

    ReplyDelete
  6. Hip is for knowledge
    Hop is for movements πŸ™ŒπŸΏπŸšΆπŸΏ‍♂️

    ReplyDelete
  7. Umetisha kaka mkubwa apo kweny album nilikuw najua utakuwa umeweka na ya kendrick

    ReplyDelete
  8. Bless up bro.let keep pushing 2025

    ReplyDelete
  9. HIPHOP πŸ‘ŠπŸΏ

    ReplyDelete
  10. Nakubali sana brother. All the best tufunge mwaka salama @dzstvn

    ReplyDelete
  11. Appropriate dizasta vina

    ReplyDelete
  12. This is Great πŸ‘

    ReplyDelete
  13. Umenikumbusha move moja ya Michael B Jordan inayoitwa just mercy anyway be blessed bloody πŸ‘ŠπŸ’―πŸ’―

    ReplyDelete
  14. Mjukuu wangu dizasta nakuombea uishi maisha marefu maan wew ni chakula la ubongo wa wengi

    ReplyDelete
  15. πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ™

    ReplyDelete
  16. Much appreciation Vina

    ReplyDelete
  17. Mkubwa umejua kuishi uhalisia ,unatupa nondo nyingi kumbe sanaa yako imestawi mno

    ReplyDelete
  18. Much respect Dizasta vina ✊✊

    ReplyDelete
  19. Others just rap for the money, while you do it to educate the masses, Cheers Mr Vina.

    ReplyDelete
  20. "Kanuni mbaya zikienziwa wafalme wabaya wakiwekwa na maadili mabaya yakiwekwa na watu ni watu wenyewe nd wataangamia"πŸ™Œ nguvu ni pale unasababu yakufanya kitu au aufanyi

    ReplyDelete
  21. Msaani wangu pendwaa 🫑🫑🫑

    ReplyDelete
  22. πŸ™πŸ™ Blackmaradona na mm nikavisome na movie nikazicheki nipate madini

    ReplyDelete
  23. Na nyuma kuna ringleeeeeeee

    ReplyDelete
  24. πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

    ReplyDelete
  25. The ancient storyteller

    ReplyDelete
  26. Old school moviesπŸ“Œ
    Your relentlessness in reasoning ilifanya niamin Hopsin unamsklza, finally proven.

    Tho kaka ikikupendeza tunaomba tupate album pia mwakan. ASANTE

    ReplyDelete
  27. Hongera sana kaka, matumaini yangu ni kuwa maarifa uliyoyapata yatakuwa Chachu ya wewe kufanya bora zaidi....

    ReplyDelete
  28. Dizasta vina the only one for learning

    ReplyDelete
  29. Bro mziki wako umefanya jamii kuishi kwa kufata hasiri asa kwa vijana wengi amebadilika kupitia wewe.. kila kijana dizasta vina

    ReplyDelete
  30. Nimevutiwa na hili, umenihamasisha, ngoja na mimi nijiwekee tabia ya kusoma vitabu mwaka unaokuja 2025 In Shaa Allah

    ReplyDelete
  31. ,πŸ‘ŠπŸ‘ŠπŸ‘Š

    ReplyDelete
  32. Tuko pamoja sana bro mwaka umeisha ulituburudisha na Albam yako bora AFF big up sana Maradona mweusi

    ReplyDelete
  33. Medulla πŸ™Œ.

    ReplyDelete
  34. Maana halisi ya dizasta na vina vyake..; najua si Bure Kuna pishi litakua jikon

    ReplyDelete
  35. Knowledge knowledge

    ReplyDelete
  36. "Wapo wavivu hata wapatwe na dhiki/wako hoi hawatoboi hata uwape matrick/ni marafiki, na wanaita wanawake mabitch/utadhani hawatapata mabinti"

    Nasoma huku nasindikiza na BEST FRIEND hapa😁😁

    ReplyDelete
  37. Awesome, I think I got something to watch this Xmas.

    ReplyDelete
  38. Young maradonaπŸ™ŒπŸ»

    ReplyDelete
  39. Pongezi kaka kuchukua mda wako kufanya tathmini ya kile ulicho kivuna katika makala hizi tofauti tofauti ambazo zinatupa mwanga na sometimes changamoto ili tufikiri nje ya Box, mimi binafsi nina tabia pia ya kufanya nukuu ya baadhi ya statement ambazo huwa za kuvutia na challenging nimefurahi kuona pia nina nukuu kama yako kutoka katika movie ya Schindler's List. Kuhusu Nguvu.
    Hongera once again kwa tathmin bora ya 5☆

    ReplyDelete
  40. Salute mkuu, ndomana unashiba sana content, pamoja since day one @Dizastavina

    ReplyDelete
  41. Usichoke kutuelimisha..

    ReplyDelete
  42. We always live once

    ReplyDelete
  43. Kaka Album yako The father figure ndio kwangu imekuwa bora zaidi kwa mwaka huu. Daima nitakubali mziki wako.

    ReplyDelete
  44. New project lini mkuu?

    ReplyDelete
  45. Appreciate sanaa broo unatupa madinii mengii sana let's push 2025

    ReplyDelete
  46. Mapinduzi halisi na mhadhiri..consious sana hizo albums

    ReplyDelete
  47. Hiyo ENEMY ni moja ya movie yenye Funzo kubwa sana, niliitazama mara tatu ili kuweza kuielewa vyema, ukiiendea pupa unaweza kusema ni bored movie lakini ukituliza akili utagundua ni movie moja muhimu sana na yenye ujumbe muhimu sana, nimependa ulivyoielezea.. PEACE

    ReplyDelete
  48. This guy himself, his lifestyle is far from many men

    ReplyDelete
  49. Dizasta vina πŸ™Œ

    ReplyDelete
  50. BLVCK MARADONA FUNDI

    ReplyDelete
  51. You really pay the price for greatness,keep on pushing Vina

    ReplyDelete
  52. Mmmh I agree your the best rapper in the 🌎
    πŸ™‰πŸ™‰

    ReplyDelete
  53. I really like to search right knowledge like you bro ...ntajaribu kufanya kufanya review ya hii summary yako hope I will learn a lot of things

    ReplyDelete
  54. 🫑Jesusta

    ReplyDelete
  55. Chakula cha ubongo
    Nakubali Dizasta

    ReplyDelete
  56. Dizastavina ni moja tu

    ReplyDelete
  57. Chakula cha ubongoπŸ”₯

    ReplyDelete
  58. Vina ni mmoja tuuπŸ’₯

    ReplyDelete
  59. The Brain, VinaπŸ™Œ

    ReplyDelete
  60. You lead we follow, much respect edger we love the greatness of your perfect work.

    ReplyDelete
  61. I got something here we must have a time to learn from many source..thanks for open my mind

    ReplyDelete
  62. love for dizasta vina

    ReplyDelete
  63. Respect bro ❤️✊🏾

    ReplyDelete
  64. Nothing to say, but bro unaijua Sanaa

    ReplyDelete
  65. Kaka hapa no comment

    ReplyDelete
  66. Nafurahi kuona maalim Nash unamsikiliza

    ReplyDelete
  67. da mwanangu wana meng yakujifunza kwako hongera

    ReplyDelete
  68. Some one from no way vina πŸ˜€πŸ–️

    ReplyDelete
  69. Fantastic Bro πŸŽ™️

    ReplyDelete
  70. Chakula ya ubongo from dizastavina

    ReplyDelete
  71. Hii kubwa sana, Asante Kwa chakula cha ubongo

    ReplyDelete
  72. WE STILL NEED YOU D

    ReplyDelete
  73. Maradona mweusi umetisha

    ReplyDelete
  74. Akuna Mc wakukufikia Dizasta vina Green city tumepata kichwa sahihi kwenye mziki wa Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ @dizasta vinaπŸ”₯πŸ”₯

    ReplyDelete
  75. Dizasta ni shule ya mtaa nzuri hii

    ReplyDelete
  76. Real dope panoramaπŸ”₯

    ReplyDelete
  77. Inspire our generation
    #D vine become an artist and living philosopher ningekua kiongozi was sanaa ningependekeza nyimbo zako zitumike mashuleni #tatto ya asili #shaidi

    ReplyDelete
  78. Baba me sina la kusema wew ni namb 1 kwasas Tz nzima

    ReplyDelete
  79. Thanks for sharing!

    ReplyDelete
  80. masterpiece 🎯

    ReplyDelete
  81. More blessing brother

    ReplyDelete
  82. Nizaidi ya pro brother Elim unayotup

    ReplyDelete
  83. nakubali sana bro kaz zako

    ReplyDelete
  84. πŸ™Thanks kwa kutupunguzia knowledge me naelewa sana books

    ReplyDelete
  85. New book certified storyteller dizasta vina

    ReplyDelete
  86. Ni maunyamaa tuh bro

    ReplyDelete
  87. Schindler List ni nzuri sana. Hii essay ya Ujamaa inapatikana mtandaoni?

    ReplyDelete
  88. Sharing is caring..nimejifunza mengi Sana kwenye hili andikoo.

    ReplyDelete
  89. Thanks for sharing man- madini Kama haya isingekua fair kubaki nayo mwenyewe πŸ‘ŠπŸΎ

    ReplyDelete
  90. Black maradona πŸ”₯

    ReplyDelete
  91. Thanks for sharing,

    ReplyDelete
  92. Mwaka 2024 umetuzawadia AFF tulionunua album hakuna cha kujutua mule ndani hata kidogo. Ni bless kukufahamu black maradonna. #HipHop

    ReplyDelete
  93. Nafikiri hii ni moja ya article bora niliyosoma boxing day

    ReplyDelete
  94. Good article kutoka kwa extraordinary man✌πŸΎπŸ’«vina πŸ‘‘

    ReplyDelete
  95. Hongera kwa juhudi, utabaki kuwa bora na Muumba akuzidishie.

    ReplyDelete
  96. We ni professor tungo kaka umetufanya tuishi kwa mwenendo wako kweny mazingira yetu tunayoiahi πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

    ReplyDelete
  97. Your music has my heart, bro! It’s truly healing. I always turn to your tracks as part of my therapy routine. Keep shining BLACK MARADONA ✊️

    ReplyDelete
  98. Pongezi & shukrani sana kwa ku-share knowledge nasiπŸ™πŸΎ♥️
    On top of that, binafsi nimekuwa nikijifunza mengi sana from your works....umeniongeza sana uelewa kuhusu fasihi, ujuzi wa maisha na uwezo wa kupambanua mengi ya kidunia. God bless you bro 🀝♥️

    ReplyDelete
  99. thank you for priceless knowledge dzstvn

    ReplyDelete
  100. Kaka nakubali sana kazi zako

    ReplyDelete
  101. DIZASTA VINA (GOD IN PERSON)

    ReplyDelete
  102. Hongera Mzee ata ambao atuku baatika kufika ngazi za juu kielimu unatufungua kiakili zaidi ubongo unapata kitu kipya chenye tija

    ReplyDelete
  103. We ndiyo king wa Swahili rap au black maradona

    ReplyDelete
  104. kuna kitu nimejifunza kikubwa sana bro dah

    ReplyDelete