VITABU
Mwaka huu nilisoma vitabu vitatu na hii ndio review yangu kwa ufupi kwa kila kimoja.1. Ujamaa - Essay on Socialism - The late Julius K. Nyerere
Kitabu kilichapichwa kwa mara ya kwanza mwaka 1961, na kufanyiwa marejeo mara kadhaa na baadaye kutafsiriwa kwa lugha ya kiingereza mwaka 1968. Nilikisoma kwa mara ya kwanza mwaka 2013 lakini nikawiwa kurudia sasa nikiamini kuwa na uwezo wa kuelewa maudhui yake kwa mapana yake. Kwenye nakala hii mwandishi anajadili maono ya hayati Baba wa taifa Julius Kambarage Nyerere kuhusu wazo lake la kuwepo kwa aina maalumu ya ujamaa inayoendana kwa asilimia mia moja na tamaduni, mira na desturi, aina ya itikadi, kiwango cha uelimikaji na mtindo wa maisha wa nchi za kiafirka (Specifically Tanzania). Wazo la aina hii ya ujamaa lilitumika kama sera kuu ya chama cha siasa cha TANU ambacho Mwalimu alikuwa ni mwenyekiti wake. Mwandishi alielezea mafanikio na changamoto ya wazo hili hasa kwenye practicability and implimitations. Nakala hii ilibaki kumbukumbu ya juhudi za mwanzo za kumkomboa mwananchi masikini baada ya Ukoloni. Hili andiko lilisanifisha kanuni muhimu zilizosimamia haki na usawa kama zilivyojadiliwa kwenye azimio la Arusha. Nukuu yangu pendwa kutoka kwenye nakala hii ni ile iliyomnukuu mwalimu kuhusu umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii kwa ustawi wa familia zetu, akisema "‘Mgeni siku mbili; siku ya tatu mpe jembe’
2. The moral Lanscape - How science can determine human values - Sam Harris
Binadamu wa karne ya 21 wamekuwa kama kitu kimoja kwa sababu ya kukua kwa teknolojia hasa kwenye eneo la mawasiliano na usafirishaji. kukua huku kumefanya dunia kuwa ndogo. Binadamu wanajijamiisha kwa karibu na kwa haraka zaidi bila kujali maeneo waliopo. Hii imekuza umuhimu wa mazungumzo kuhusu falsafa ya maadili. Mwandishi wa The Moral Landscape, Kitabu kilichochapishwa mwaka 2010, Sam Harris anajadili wazo la kuhusianisha maadili na ustawi wa maisha ya binadamu (Well-being) akisema Mijadala ya maadili haitakuwa na maana kama haitahusisha ustawi wa maisha ya binadamu na wanyama. Pia alijadili kwa kiasi gani sayansi itaweza kutupa kweli ya nini maana ya ustawi hasa kwenye eneo la afya ya akili, mwili na hisia za binadamu. Pia alijadili tamaduni na imani mbalimbali zinavyoweza kuhatarisha afya ya mwili, akili na hisia, lakini pia afya ya uchumi wa binadamu. Nukuu yangu pendwa kutoka kwenye kitabu hiki ni "Wanawake na wanaume walio kwenye hukumu za kunyongwa, wapo pale kwa sababu ya mchanganyiko wa malezi mabaya, mawazo na itikadi mbaya, imani mbaya, vinasaba mbaya au bahati mbaya"
3. Who we wrestle with God - Jordan Peterson
Kitabu hiki kilichapishwa November 2024, Ndio kilikuwa kitabu cha mwisho kusoma mwaka huu. Mwandishi anajadili hadithi za mwanzo kabisa za kifasihi na umuhimu wake kwenye maisha ya sasa. Mwandishi anaamini kuwa fasihi za zamani ni muhimu kwa sababu zinatupa picha ya mtindo wa kufikiri wa jamii za kale (their thinking process). Mwandishi pia anajadili dhana ya ukaidi, sadaka, mateso na ushindi kwa kutumia hadithi mbalimbali za kibiblia. Jordan anachagua Biblia kuelezea subject matters zake akiamini ni kitabu stahiki zaidi kiushawishi, kiumri na kiuhalisia (authenticity). Moja ya subject matter alizojadili mwandishi ni IMANI na kujitoa SADAKA (Faith and sacrifice). Anasema dunia na mapana ni kubwa sana kiasi hatuwezi kuimaliza kuielewa hivyo kwenye maisha mafupi ya binadamu huwa tunachagua vile tunaavyoona ni muhimu. Na hapo ndio Imani na sadaka vinapokuja kwani kuchagua ni kuamini kuwa upo sawa na machaguo yako na unatoa sadaka vingine vyote ili kufuata unachoona ni sahihi (cost of choices/opportunity). Mfano wa hadithi alizotumia kujadili maudhui ni ile hadithi ya Yona aliyeikimbia sauti ya Mungu iliyomtuma kwenda Nineveh kueneza habari njema, Yona alikaidi na mwishowe kumezwa na samaki. Mwandishi alihusisha hii hadithi na athari za kukimbia majukumu kwa nafasi uliyopewa. Nukuu yangu pendwa kwenye kitabu hiki ni "kanuni mbaya zikienziwa, wafalme wabaya wakisimamishwa na maadili mabaya yakiwekwa na watu, ni watu wenyewe ndio wataangamia"