–
LYRICS
–
Search for a song or choose an album and track.

A FATHER FIGURE
Dizasta Vina
A confession of a mad father
A FATHER FIGURE • Dizasta Vina
Lyrics copied!
Nilimwambia hakuna kitu ataniambia
Nikifa hakuna kitu nitamwachia
Nilimwambia anaitia aibu familia
Nilipenda mtoto ila tangu nimzae nilijutiaNilimwambia anastahili fimbo
Anastahili msiba mbaya usio na maziko
Asikae mezani asishike sahani au kijiko
Asitumie jina langu la mwisho
Nilimchukia sanaNilimwambia asiniite baba
Aliponiita hata bahati mbaya nilimchapa
Sikumpa mahitaji, hamu ya mtoto iliniisha ghafla
Alianza shule sikulipa adaWaliponiuliza nilimkana hadharani
Nikasema hata kufanana hatufanani
Nilimwambia simpendi ni bora ningezaa hata Nyani
Nilitamani nimgawe kwa jiraniNilimpeleka kwenye misa za kilokole
Nilimchapa viboko vya kutisha kwa Mkole
Habari zake zilitambaa nilipewa pole
Nilihama mitaa kuepusha watu kuninyooshea vidoleNilimuwekea mifano kadhaa ya kubuni
Kwamba kuliko yeye bora ningezaa hata Mhuni
Nilimwambia namwona kama Chawa au Kunguni
Aliniponigusa bahati mbaya nilinawa kwa sabuniSikumpenda nilihamishia chuki kwa Mama yake
Niliona laana kuleta mtoto wa aina yake
Sikutaka kumwona wala kumjua katu
Na nakiri Nilishajaribu kumuua mara tatuHakuwa na marafiki tulimtenga ndugu
Tuliamini ilikuwa ni laana toka kwa Mungu
Alinikimbia sikutaka kusikia sauti yake
Sikuwa tayari kuuafiki utofauti wakeTulimweka kwenye taasisi bila idhini
Alelewe akifanyiwa uhakiki wa kidini
Kilichofanya nimwone ni mzigo mara mbili
Ni pale taasisi zilipomshindwa kumbadiliTofauti ya haiba na hisia
Sikuwa tayari kamwe kuukubali uhalisia
Achana na vipigo vikali kumnyima chai
Ilibakia kidogo nimzike akiwa haiNilikomaza chuki kwa kutumia jadi na dini yangu
Au itikadi ya jamii yangu
Nilifurahi kuona hana mahala pa kwenda
Maana sio marafiki hata ukoo ulimtengaHawakutaka wakae naye
Vitabu vya Mungu vilishauri auwawe
Nilikesha kuomba Mungu aibadili tabia yake
Alipopita karibu nilimtemea mateNilimwita majina ya kutosha ya kishezi
Mara boga mara mboga mara shoga mara ndezi
Mara mzoga, Nyoka asiye nyooka kwa malezi
Nilitamani hata nafsi ingemtoka niimbe tenziNiliamua kufanya maamuzi magumu
Nikamfunge porini kisha nimnyweshe sumu
Nikaandaa nyezo nikanunua na kamba
Nikaenda chumbani nikakuta barua kwenye kitandaInasema
Mi ni mtumwa wa maumbile kiasili
Iliyonizidi nguvu kihisia kiakili
Natamani ingekuwa rahisi kubadili
Na kwa bahati mbaya Baba hukuwa tayari kujadiliNisamehe sana baba
Muda hautoshi kukuomba msamaha mara saba
Kwakuwa nimeshindwa kuwa jinsi we unataka
Najitoa uhai ili nikuondolee dhihaka
More From This Album
More songs from this album
Join The Family
New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.
© 2026 Dizasta Vina. All Rights Reserved.