–
LYRICS
–
Search for a song or choose an album and track.

A FATHER FIGURE
Dizasta Vina
A father figure (Official album intro)
A FATHER FIGURE • Dizasta Vina
Lyrics copied!
Natazamwa kama mgongo
Wa kuegewa kama chombo
Nikitegemewa na watoto
Lakini kwa ndani mi' ni mtoto piaMtoto wa katikati
Njiapanda kati ya
Ukweli na uongo
Ukubwa na udogo ama
Upofu na uchongo
Ama pumbazo na mwongozoKatikati ya uhalisia
Na mategemeo
Karibu na jitihada
Mbali na egemeo
Sina hesabu ya mafanikio
Kila kitu ni jukumu na uwepo wangu
Ndio hukumu yangu ya leoSina cha thamani nilichorithi
Ila nilichonacho ni kumbukumbu ya simulizi
Na picha nilizokuwa nazo
Nilizopewa na wavuja jasho
Wasakatonge wa mwanzo kwahiyo
Nigawie masikio yakoMacho yalinipa tishio lenye manufaa kwangu
Maana nilishuhudia kufanikiwa na
Kushindwa kwa mashujaa wangu
Lakini shuhuda zilinifunzaZilinifunza kuhusu Mashujaa
Wa karibu na mbali
Wenye nasibu za ghali
Au watabibu wa kuponya hali
Na nguvu ya kufukuza shali
Za wadhalimu na waharibifu
Wenye visu vikaliMashujaa walisisimua sana
Lakini wapo kadhaa waliokufa
Na hawakuacha alama
Nilifunzwa kuhusu hawaHawa mashujaa walipanda maua
Wakilea vyema yakachipua
Na wengine usingizi ulipowachukua
Wadudu wala mizizi wakafukuaMachache yaliyofanikiwa kukua
Ndege waliyachukua
Na mengine hayakuwa mahala pema
Kwahiyo yalichomwa na jua na kuunguaOooh hujui walimwengu walisema nini
Kuhusu hawa mashujaa wangu walioshindwa
Walisema Kaharibu
Kwakuwa shujaa kwa walimwengu
Ni yule anayeweza wakati wa kufanya
Lakini sio anayeshindwa wakati akijaribuKwa walimwеngu shujaa
Ni yule mwenye nguvu
Asiyеtoa chozi wakati wa uchungu
Asiyekosa au anayeonekana mtukufu
Kwa walimwengu ushujaa ni
Kuweza na sio kuthubutuKwahiyo wakati sherehe za mashujaa
Wao zikipikwa kuchochea
Hadithi za mashujaa wangu
Zilizikwa na kupoteaKwakuwa mashujaa wangu
Hawakuvaa suti zenye nakshi na kuita
Hawakuwa na viatu vya kung'ara hivyo
Hawakupendeza kwenye jaridaNi kama walipima ushupavu wa mashujaa
Kwa kuangalia afya za maua
Bila kujua afya za maua sio ubora
Wa anayeyajua pekee
Lakini kuna jua na mvua na ni
Ubashiri wa kujua lini vinakuja
Uhakika wa kesho, kesho yenye giza
Na hakuna anayeitambuaShujaa wangu alileta mlo mmoja
Kuhakikisha siku haipiti, na aliweka
Tofali moja wakati wa kujenga msingi
Alifagia barabara alipambana na
Uraibu kama kamali, ulevi na madawa
Ila hadithi yake haikuvutia gazeti
Sio sawaNi vile nimeanza kuwa kama shujaa
Wangu nimegundua kuwa sijamaliza kujua
Ni kama nimeanza kulea wakati sikumaliza kukuaNatamani kuwa shujaa mzuri
Lakini nipo hapa kujifunza
Na pa kuanzia sipajuiSipajui maana maelekezo ni mengi saa hii
Mara jikaze wewe, baba halii
Mara utapoteza nafasi, watu hawatanii
Mara kwanini usifanye kama nanihii
Ona mtoto wake amenanihiiBahari ya elimu ni pana kuushinda upeo
Kulia matarajio, kushoto mategemeo
Bado najifunza sipo mbali
Ila sijui lini nitakuwa tayariInaniwia kuweka kipimo
Cha kujua kipimo kiundani
Kupima usahihi na wito
Ninaposema hadharani
Unawaandaaje watoto kwenda mitaani
Kwa sababu kuliko kuwa mkata maua vitani
Ni bora kuwa mwanajeshi kwenye bustaniNini maana ya kuwa baba
Ikiwa bado najifunza
Kutosherehekewa nikishinda
Ila kusakamwa nikianguka?
Hata nikipendwa au nikichukiwa
Ni sawa ila si vyema nikapuuzwa
Nimechelewa ila ni vyema
Nimejua kuwa baba hazaliwi
Anaundwa
More From This Album
More songs from this album
Join The Family
New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.
© 2026 Dizasta Vina. All Rights Reserved.