LYRICS

Search for a song or choose an album and track.

A FATHER FIGURE album cover

A FATHER FIGURE

Dizasta Vina

Chupa moja ya ziada

A FATHER FIGURE • Dizasta Vina
Lyrics copied!
Kalala chini ubongo na fuvu vimetengana Hatoi sauti hana hata nguvu ya kulalama Macho yetu yanagongana ya kwangu yanaona haya Natamani kufumba maana naona uchungu kumtazamaNi butwaa siwezi eleza hali yake Mifupa imezagaa kadhaa haipo mahali pake Waungwana wamejaa wanauliza ka' mi' timamu Damu nyingi nataka niamini ni filamuHata nikifumba macho naona jambo hili hili Nafsi yangu inahofu na inatukana kwa siri siri Ameumia siwezi kumtazama mara mbili mbili Mguu mmoja umetengana na kiwiliwiliKweli nimeamini utu wa mtu ni uhai wake Mja amelala watu wamewahi karai lake Wengi wanatabiri tanzia bila kuficha Wema wanalia na mabazazi wanapiga pichaAmechanika nyama kuonyesha nyama si tunu Anapata maumivu kabla hajaikumbata huru Anaonyesha kuwa mwili ni kasha lisilodumu Na kujua siku ya uhai kutoka ilivyo sumuMtoto wake analia ameisoma ajenda Kuwa baba uhai umetoka na roho yake ishakwenda Anahitaji uthibitisho na picha inajieleza Ananiona mimi nami sina ninachokiwezaNatamani niamke nigundue picha nicheke Au labda naota ndoto ya kutisha nikeshe Huku wapita njia wakipiga kelele Kuona mtoto anakuwa yatima mileleChupa moja ya ziada Chupa moja ya ziadaNilipigiwa simu ikisema njoo baa Maana mtungi wa nyumbani haunogi Nikalewa kisha nikataka kuondoka Mpumbavu mwingine akasema one for the .....Chupa nikazipanga panga Mfuko ulipokauka wakanijaza Nikanywa nikijitapa kama mjanja Wana wakipiga kelele kuniita (mwamba mwamba)Sikio la mlevi likashika habari Sifa walizonipa zikanishika hatari Sikuwaza kuwajibika kuwa nani nitamuumiza Nilikuwa mbinafsi kiasi nilishindwa kujaliLabda ningebakia kwenye kijiwe nongwa cha Biafra Ninywe kahawa nikisikiliza soga za siasa Ningekunywa kidogo labda nisingerudia Nimeua mpita njia sababu ya chupa moja tu ya ziadaNimefanya kosa na muda unakwenda hasa Hasa nitaongea kipi? kipi nitaeleza sasa? Sababu chupa moja tu ya ziada Mke anamkosa mume aliyempenda Mtoto anampoteza babaMaji yameshamwagika nani wa kunifundisha lugha? Niseme kwa nani ama nani wa kuunganisha nyufa? Nani wa kuujuza umma kuwa nami najuta nafsi? Nani asimamishe siku kisha akaurudisha muda?Malipo gani yakurudisha pumzi kwenye mwili Uamke tena? uhai hata kwa hela tu haukopwi Adhabu gani itamfaa mpuuzi kama mimi Asiyejua maana ya pumzi? Maana hata jela tu hainitoshiHata nikiamua kufunga na kuuungama Siwezi kuzuia uuma wa watu wakiungana Kuamua kumwaga damu kwa mja nilie na laana Nife nilipe deni kwa hii dhuluma niliyoifanyaMuda umesimama moyo unaingia baridi Nimemgonga na gari picha inanijia saa hizi Mja anakata roho picha inayoingia zaidi Ni kuona vibaka wanaiibia maitiChupa moja ya ziada Ziada ziada ziada ziada ziada Chupa moja ya ziada

More From This Album

More songs from this album

Join The Family

New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.

© 2026 Dizasta Vina. All Rights Reserved.