–
LYRICS
–
Search for a song or choose an album and track.

A FATHER FIGURE
Dizasta Vina
Hatia VI
A FATHER FIGURE • Dizasta Vina
Lyrics copied!
Salamu baba mi mwanao
Naandika waraka kwa maana hutaki vikao
Nahitaji majibu nikihisi ni haki yangu
Najisikia vibaya kusikia unaishi na sina ngaoNimeshika kalamu haya maandiko
Yametoka mahala timamu palipo wito
Sijatumwa na wenzangu hii ni akili yangu mwenyewe
Waraka huu ni salamu zangu za mwishoNina akili najua mambo yanapokuwa mrama
Natambua uhalisia nazitambua njama
Pengine nitachokisema kitazua laana
Nitaibeba lawama kwa kujifanya najua sanaNdugu zangu wanachosema sisawiri
Mpaka wanahisi nimeanza kuchezwa na akili
Hata wakitaka kunitenga sibadili
Ulinitenga jana siogopi kutengwa mara mbili babaMajirani wanatamba kukuongelea
Wakisema sina baba na kazi ya kukusemea
Na ukweli ni kwamba ni utata sana kukutetea
Maana shida ilinibana na baba haukutokea jeUtachukia nikiegemea penye power
Au utanipa hatia mikono michafu niende nawa
Nipo mbele yako kamwe siigizi uwepo kama wewe
Basi jibu kero zangu twendе sawaJuzi nilikuhonga maua, Jana nikakuhonga na tena
Subira gani isiyo na heri shaabash
Nimechoka kuchomwa na jua
Jionyеshe leo nimechoka barua
Nimechoka baruaBarua zako zinahubiri ushindi
Kutangaza vita wakati mtutu tu haushiki
Na cha ajabu maadui ni wa kurithi
Chanzo ni kitendawili nilichokisoma kwenye hadithiNjoo ulee wagonjwa ndo' uongee kuhusu upendo
Tuvae bendera moja ndio uongee kuhusu uzalendo
Msamehe aliyekufanya uondoke ndo' uendeelee
Kuhubiri kutubu kuhifadhi na kusameheJenga daraja baba mahusiano yanavunjika
Hamna faraja huoni wanao wamekaza ndita
Jenga imani tena kwa wote waliogadhibika
Jenga kama ambavyo uliijenga hii nyumba kwa siku sitaHaukuja tulipopita kwenye
Miaka 400 ya utumwa njaa maradhi vita giza nene
Nipe sababu moja vipi nikujali vipi nikupende
Sababu moja tu kukusikiliza weweNyumba uliyotupa ina twiga ina ndovu
Majirani warembo wenye figa na vitovu
Vinavutia, kuna dhahabu kadhalika
Zinatutajirisha ila zinafanya tuwe waovuHuu uchafu atatetea wakili gani
Siri ipi na asili zetu hazilingani
Japo akili mali sio siri asili ghali
Tunamwagana damu kugombea rasilimaliTunaisha kwa wivu wetu
Tunasita kwa uvivu wetu
Tunazikwa na mbinu zetu
Tunapikwa na kinu chetuTunasita kushika insha
Tunapitwa na wapita njia
Umoja unavunjika huku
Tumeshikwa na simu zetuSina tofauti nna watoto kama wewe
Napata changamoto kama wewe
Kama soja kwa ajili yao napambana naposhindwa
Tunateseka pamoja Kwani sina roho ndogo kama weweAsante kwa ulezi dhanifu
Asante kwa kuniandikia sheria za kishenzi
Kwenye pegi nadhifu asante kwa kuniacha stendi
Nikisubiri mapenzi ya ahadi nakesha nikienzi wasifuAsante kwakuwa mbali nami
Kiasi nina shaka kuwa haujui nina hali gani
Umeacha barua ndefu ambayo sijui kama yako
Au ya kufoji na bado inahitaji mkalimaniOna Napanga mipango ya kijinga
Ona naghafirika nafanya uliyopinga
Ona napinda napika chuki wenzangu
Wenye nyumba ndinga maana mimi ngano tu inanishindaHuko mbali umejitenga nashanga
Haujui kinachosemwa na jamaa
Haujui usafi ni ndoto, ndoto iliyotengwa na ridhaa
Haujui ni ngumu sana kuwa mwema ukiwa na njaaHaujui kuhusu adha za dunia
Haujui kero maana maudhi yalipokupata ukakimbia
Haujui kuhusu kifo na magonjwa haujui kuhusu
Insha na maandiko haziwezi tibu hivi vidondaNdugu zangu umewajenga kwa vpaji
Wapo kadhaa umewapa pesa za mitaji
Wengine warembo wenye vyeo wenye hadhi
Sisi tusio na hali tulalamike kunyimwa hakiImechafuka taswira inaenda slow focus
Pengine its all bogus
Pengine I'm mad
And I'm talking to my own consciousLabda haupo ni hadithi tu
Na kama ulifikia kifo ufalme umefika mwisho
Haurudi tena so nawaza
Lini utakuwa mwisho wa uhanithi huuUzazi sio simple but I still care
Nina watoto shida zipo and I'm still here
Matatizo yanapokaba kwenye shingo sikimbii
Napambana mpaka mwisho like a real manSio kosa langu kutokuwa na uhakika upo
SikujuI sura maana hauna picha Google
Nipe ishara kuwa unaishi hata nikituma
Bakshishi niwe ninajua kuwa zinafika hukoWenye majoho rangi nyeupe na dhahabu
Wana barua zako za tafsiri za kiarabu
Wanasema wanakujua kuliko ninavyokujua
Nikiwatilia shaka wananiita mwanaharamuJe ni kweli uliwapa uwakilishi
Ni ngumu kuwasadiki hasa ukiwadadisi
Kama wanaongea uhalisi au wanachonga sera
Sometimes hawafundishi wananiomba helaThibitisha hizi hifadhi si uwongo
Uliowaacha wana nishani za uozo
Wakificha sura kama ulivyoficha wewe
Utawaadhibu kwa maji na moto
Wakati unahubiri msamahaNina maswali bado
Halahala sikukemei
Nashangaa wenzangu wanakesha
Wakiimba utukufu wa dhambi zako
Au ndo' mkubwa hakoseiNimeelemewa na dhambi
Baba mzazi unasema sina hadhi
Unajua wasifu unajua majibu
Umenizaa dhaifu unategemeaje niwe msafiKwanini usije ili tujue moja
Uuonyeshe uso wako ili tufunge hoja
Kwanini usijionyeshe tufurahi nafsini
Tujue kipi halisi kipi sogaWanao wanaweka mipaka wakivutana
Wanabishana kila kikao wakikutana
Wameishi bila uwepo wako juzi na jana
Swali ni kwamba utaonyesha hasira wakikukanaUlinizaa kwa matakwa yako
Nilisimama kwa ajili yako ni zamu yako leo usimame kwangu
Sina usafi kama wako hautaki nilitaje jina lako
Kwanzia sasa usilitaje languNilihitaji jibu moja tu sio picha mia
Umeamua kujificha so najificha pia
Nimekutafuta vya kutosha nimechoka
Nipo hapa ukinihitaji unajua pa kunipata dear..father
More From This Album
More songs from this album
Join The Family
New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.
© 2026 Dizasta Vina. All Rights Reserved.