LYRICS

Search for a song or choose an album and track.

A FATHER FIGURE album cover

A FATHER FIGURE

Dizasta Vina

Mbuzi

A FATHER FIGURE • Dizasta Vina
Lyrics copied!
Verse 1 Mbuzi alipata wadudu kwenye kwato Iliathiri furaha na nguvu alizonazo Mchungaji alihakikisha mbuzi ananawa Aliondoa wadudu wote kisha akamweka dawa Alikampangusa chawa akampa chakula kwa wakati Akamjengea chumba kwa nafasi Ajisikie huru, Akashika ratiba na itifaki Muda ukapita afya mbuzi ikatamalaki Mtaa ikahamaki ukasukwa uvumi Kuwa bwana Kheri Anatoa muda kisha sumni Japo hali yake ya uchumi ilikuwa ni duni Aliuza matunda mboga chache na kuni Hakuna siku mbuzi alipiga kelele kwa njaa Watu walimwonea gere balaa Alinawiri kwa kilele cha umaridadi Majambazi walipiga misele kadhaa Na usiku hauwi mwanana akisikia mbiu Mbuzi akilalama kwamba anahisi kiu Mchungaji alikuwa macho Akatambua kuna magonjwa nyemelezi akavumbua chanjo Mbuzi aling’ara alinona Manyoya yalitawala kuashilia afya kila kona Hakuwepo hata mwanga mmoja wa kuroga Hata Waliojaribu kuchanja walikomaVerse 2 Najiuliza maana ya upendo nini Mpaka uwe na kingi ndio ushee? Au pesa kipindi michango ya sherehe? Au mzazi anayetamani mtoto uendelee? Ndio maana anakulea ile umlee Inasadikika kuwa upendo wa kweli ni kujali Mama mzazi homa ikikushika tu halali Tabasamu analokupa unaposhika Masarali Ungekuwa hai ingekuwa kutoa mimba ni halali? Wazalendo wanahitaji hela na nyadhifa Wanalipwa kutetea sera za taifa Wadini wanakumbatia itikadi na imani yao Mpaka wanamwaga damu za wenzao Na mapenzi kwenye timu inapoingia mtimani Unaumia inashika mkia na hauhami Kufichiana dhambi tabia wanayoisifia masela Au mjeshi anavyofia bendera? Nani anajua siri ya kupenda penda? (Ni) kujitoa sadaka kwa ajili ya mwenza? Wapo wanaosema kuwa kupenda ni ushupavu Wanaumizwa wanachukia wanaandika vitabu Ukijua mwenza wako ana mtu anampenda Utampa nafasi aende upige moyo konde? Mama yako akifariki na una dawa ya kusahau maumivu Swali ni utakula vidonge?Verse 3 Je upendo wa kweli ni mpaka aagize Mungu? Aliyesema ufuge paka alafu umchinje kuku Amemmtoa mwanaye kama mdhamini msalabani Awafie watu ambao dini hazifanani Bado Mawazo yananisumbua nasinzia Nawaza ingekuwaje tungechagua familia Je mtoto angempenda baba angekuwa lofa? Au Baba angemchagua mtoto kama angejua ni shoga?Wanandoa tungekuweka kwenye Time Chamber Muda urudi ungemchagua patner wako tena? Wangapi wanawish wangepita sehemu hii? Wangapi wangemchagua Justin Bieber na Jay Z? Kabla ndoa haijakufunga pini Jiulize kama mkeo angekuwa na wewe ka' ungekuwa chini? Licha ya hizi nyimbo zinazofanya watu walie sana Washikaji walingoja niwe msanii ndio niwe mwanaPengine inabadili maana ya upendo Na kuacha swali upendo je ni haja au matendo? Mchungaji alifuga mbuzi alifuga na ajenda Alimjali lakini si kwa sababu alimpenda Kwani ilipofika sikukuu alitoa vitu Sufuria jungu kuu akanoa visu Yule mbuzi mzuri aliyenona sana Ndiye aliyechinjwa na adhuhuri alichomwa nyama

More From This Album

More songs from this album

Join The Family

New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.

© 2026 Dizasta Vina. All Rights Reserved.