LYRICS

Search for a song or choose an album and track.

A FATHER FIGURE album cover

A FATHER FIGURE

Dizasta Vina

The last confession

A FATHER FIGURE • Dizasta Vina
Lyrics copied!
"Baba, let me get this clearly, ni wewe kweli umefanya hivi? Na kama ni wewe, ni kwanini ulifanya hivi? Unajua, hatuwezi kukusaidia. Sio dada Mori au kaka Levo, ikiwa hatutajua the real story"Nilipozaliwa nilijua ulimwengu ndio utanionyesha dira Sikujua dini wala kabila Sikuwa na itikadi desturi wala mila Wala chama, niliujua upendo kabla ya hiraNilionyesha tabasamu hata kwa ambaye simjui Kabla ya ulimwengu haujanipa maadui Kabla sijajifunza kuchagua Niliujua umoja na ulimwengu ndo' ulionifunza kubaguaNafsi haikuweza kutamani Nilifundishwa pesa ina thamani Kabla ya utu, nilijali nilimpenda Mkyuba na Mjerumani Hata kubagua rangi nilifunzwa tu ukubwaniSikutunza kisasi nilipofanyiwa njama Ya dunia yalinighasi nikamkimbilia mama Jamii ilizembea walimwengu wakashindwa kunikanya Na wazazi wakanitishia laanaSikuujua uongo sikuujua ufitini Nilifunzwa na hii dunia sikuwa mchoyo kwa idhini Dunia ilinipa ndugu wakanidhamini Kabla kunifundisha utu wakanirithisha diniNiliigawa thamani kwa kuzingatia upendo Kabla dunia haijanifunza kuutamani urembo Wakati mdogo sikuijua mipaka ya wahisani Nilivunja nikaenda kucheza mpaka kwa jiraniEeh!! Sikuona ishu aisee Kumbe jirani alikuwa na bifu na mzee Mzazi alinipa kula sikuweza kuihoji haki Bila hatia nikashiriki ugomvi wa wazaziNdipo nilipoijua chuki Nikajua maana ya mipaka ya Marekani na Urusi Sikujua kuongea nikapewa lugha ya Matusi Na kabila la Kihutu ili nimtukane MtutsiNikamjua ndugu wa upendo anaitwa wivu Nikayajua majivuno kisha hasira kisha bifu Nikafichwa ustaarabu nikafichwa haya Nikapewa nguvu za miguu niende kuutimiza ubaya"Ah Baba, unajua unaweza kwenda jela miaka mingi sana? Hivyo kuwa direct basi. Ukiweka pembeni falsafa zako, tunahitaji utuambie ukweli Why? why uliamua kufanya hivyo? ehh? kwanini yaani?"Asili imenipa macho nashukuru Nione mabaya matamu nione mazuri yanayonidhuru Wazuri wanaojiremba niwapende Ili nitoe jasho kisha nije niwape pesa wanitendeUjirani uko wapi? siku hizi hatuchezi pamoja Hatupigi soga tunawekeana mageti Ah hakuna kuombana chumvi Kwakuwa kuna fensi ukuta mkubwa na vihunziTunafuga vikosi vingi vya kininja Mbwa na majeshi na walinzi kujilinda Mwanzo niliogopa simba Sasa nafunga mlango maana hata binadamu ananiwindaNimekubuhu nimekinai maudhi Naona mstari mwembaba kati ya uhai na mauti Sikuchagua hasira au kinyongo kunishika Nikalambisha udongo watu sitaWa kwanza nilimpiga risasi mara tatu Sikuuliza maana hakuvaa gwanda kama langu Kiongozi akasema nisipigwe na bumbuwazi Kutoa uhai wakati wa vita si uuajiNikajuana na mtu wa pili Mungu wa dini yangu alimwita huyu kafili Tulichukiana kiasi alitaka kunipiga Nikamuwahi maana imeandikwa vita ni vitaWa tatu alisahau chake changu changu changu Njaa yake ilimleta kwenye shamba langu Nikamkamata nikamziba mdomo asilete methari Nikamfungua macho na sikio aujue ubepariWa nne na watano waliniletea ushenzi Cheo kilikuwa kidogo wakati tulikuwa wengi Ili wasije kufukua maiti, nikamuua wa sita Alikuwa shahidi

More From This Album

More songs from this album

Join The Family

New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.

© 2026 Dizasta Vina. All Rights Reserved.