LYRICS

Search for a song or choose an album and track.

A FATHER FIGURE album cover

A FATHER FIGURE

Dizasta Vina

Theluji

A FATHER FIGURE • Dizasta Vina
Lyrics copied!
Anachota kwa vidole viwili Anachemsha kwa kijiko inanawili Inakuwa nyevu, anachukua bomba la sindano anaivuta Inajaa kisha anadunga mwiliAkili inahama anaita stimu Ladha tofauti, sawa na sukari na ndimu Kila stimu ikiisha anajiongezea Anazoea mwili unanasa anaanza kubobeaAnajaribu kuacha anairudia Mwili unamlilia uraibu unamvizia Hataki uhalisia maana haujamvutia Anajianzishia uhalisi bandia AnasemaMwili unapoa akili inatosha tufani Kihali gani chombo akidondoka rubani Alitaka furaha, furaha imegota tutani Dawa inampa amani, amani aliyokosa nyumbaniAnapoteza sura ya kisomo Anapoteza kazi, hamu ya chakula na ngono Raha anayoipata inakuwa siri yake Kiasi anauza mali kukidhi haja za mwili wakeMuuzaji anaendelea kuuza Serikali inaendelea kuzuga Jamii inaendelea kuvunga Washikaji wanaendelea kuvuta Mtaa unaendelea kufaUsimuuzie madawa mwananguNajua hii kazi inakupa mafao Tafakari yatamkuta mwanao Usimuuzie madawa mwananguStarehe yake mpya inamvunja pochi Inamaliza afya lakini inamfuta chozi Inamweka mahala pasipoguswa na Mwokozi Bahati mbaya damu inawasha anakuna ngoziTheluji inamfikisha mbinguni vyema Anaihusudu hali Kiasi anashuka anaiba mpaka mali ili arudi tena Anaisujudu ganziAlikuwa na mchumba Wali-share all the nice things you know? Dinner dates Ice creams Walienda kwenye bata za mjini, kumbi za movie Kuangalia sijui The black Panthers sijui The VikingsLeo yupo ila hatamaniki Haangaliki Bora angekuwa malaya au mlevi wa bapa nyingi Ningeelewa, leo ngada zinamfanya anakata ringiWanasiasa wanabishana Mchungaji ibadani na Polisi ofisini Wafanyabiashara wana idhini Na mtaani madawa Yanaendelea kuwalaza chini vijanaNajua biashara inakupa mafao Kiasi kwamba unawaza jinsi ya kutupa mbachao Lakini usimuuzie ngada mwanangu Labda kesho yatamkuta mwanao, just think about itLabda hauna elimu sana Naomba tuongee ka' wazazi maana Nimeuchoka huu ubazazi Unaofanya nahisi umepitwa na wakati Na unajua nakuheshimu mwanaSina nguvu ningekupeleka mahakamani Ila uchumi wetu haufanani Mpambanaji leo nashindwa vitani Namzika mwanangu 'asa mi' nitazikwa na nani?Swali, una nguvu? Ndio Haufanyi chochote kutafuta suluhu? Sio Hauko mahabusu, familia yako tukufu Kwa hiyo unahisi haya mambo hayakuhusu, au sio?Usimuuzie madawa mwananguLabda hii kazi inakupa mafao Tafakari yatamkuta mwanao Just think about it

More From This Album

More songs from this album

Join The Family

New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.

© 2026 Dizasta Vina. All Rights Reserved.