LYRICS

Search for a song or choose an album and track.

A FATHER FIGURE album cover

A FATHER FIGURE

Dizasta Vina

Utaliimba Jina Langu? (ft G Nako)

A FATHER FIGURE • Dizasta Vina
Lyrics copied!
VERSE I Sitauona uzuri wa mataa Maua na uturi au usafi wa suti nitayoivaa Mtajadili kama nilifunzwa chuki na hii njaa Au msamaha niliomba baada ya kuivunja mioyo kadhaa Mikono yangu haitaishika sayari Historia nitakuwa nimeimaliza tayari Naenda upande wa pili, asili itanipiga kabali Nitakuwa nimeimaliza safari Maombi hayatakidhi nisimame soja Nanyi mtaijua hadithi hii ya upande mmoja Pesa na ustaa hautanibeba Itaandikwa "mwisho wa kila shujaa ni jeneza" Siwezi kimbia udhuru hata nikibadili njia Nakuwa huru dhidi ya kufuru za hii dunia Mwangaza hautafika himaya yangu Je mtafurahi nikifa ama mtaliimba jina langu?Siku hii iwakumbushe kuwa kesho mbali Iwakumbushe havina maana pesa mjengo mkali Vyeo urembo na pesa nyingi Ni kiburi cha hii pumzi, pumzi ambayo ni temporary Sijui Nitamwachia nani mama yangu Ikiwa, nitaacha dini, itikadi ya chama changu Cheo changu hakitakuwa na maana tena Nitalala gizani japo mtajua nimelala pemaCHORUS Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu Na kweli Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu Na kweli Dunia inashindwa kunilinda Dunia inashindwa kunilinda Dunia inashindwa kunilinda Dunia...VERSE II Nitalala sitahisia karaha zako Sitasikia matusi sitasikia msamaha wako Sitasikia kicheko au kilio cha unafiki Ubongo hautatafsiri mawimbi ya sauti yako Nini maana ya chuki yako kwangu ikiwa Siwezi amka hayafungukia macho yangu Nitakuwa mbali peke yangu futi sita Hata kivuli hakiwezi kuwepo kando yangu Ufedhuli ni kibari cha hii nguvu Ya nyama na mifupa ambayo ni mali ya wadudu Ipo siku utaimbiwa pambio na wadau Kisha Ndugu watagawana salio na kusahau So, nataka nikifa msinidai Msilie msherehekee niliyoyafanya nikiwa hai I wonder kama mwangaza usipotimba himaya yangu Je utafurahi nikifa ama utaliimba jina langu?Minara yangu imara itadondoka nayo Sauti yangu ya gharama nitaondoka nayo Masikini roho yangu mimi Itaenda wapi pindi mwili utakapogusa Udongo mkavu chini Mwangaza hautafika himaya yangu Je mtafurahi nikifa, ama mtaliimba jina langu?BRIDGE Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu Na kweli Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi...CHORUS Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu Na kweli Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu Na kweli Dunia inashindwa kunilinda Dunia inashindwa kunilinda Dunia inashindwa kunilinda Dunia...Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi (Dunia inashindwa kunilinda) Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi (ni dhaifu na kweli) Dunia inashindwa kunilinda Dunia inashindwa kunilinda Dunia inashindwa kunilinda Dunia...

More From This Album

More songs from this album

Join The Family

New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.

© 2026 Dizasta Vina. All Rights Reserved.