LYRICS

Search for a song or choose an album and track.

A FATHER FIGURE album cover

A FATHER FIGURE

Dizasta Vina

Wachezaji wa timu

A FATHER FIGURE • Dizasta Vina
Lyrics copied!
Wanasema duniani kuzimu Kwanini ukeshe kushika protocol wakati Ulaji muhimu Watu wanachohifadhi ni mbinu Kucheza kulia kushoto ila wote ila wote Ni wachezaji wa timuChumba kilijaa njemba za kisasi Walipanga vifaa ka' wanakwenda kwenye kazi Palikuwa jitu juu meza yenye glass Limeshika tissue kusafisha chemba ya risasiWalijaa na maninja na ma bouncer Wamevimba wenye sura za kutisha Wamekausha Wamegadhibika mpaka amani ilijificha Nilihisi mkojo unatiririka kwenye trouserSura za kutisha nafuu devils Crate zimemwaguka utadhani sikukuu kesho Kulikuwa kumejaa camera full angles Huku warembo waki-twerk twerk juu ya pool tableHuku watemi wa ngenga wameketi Mwonekano wa Rostam Bakhrеsa na Mengi Palikuwa na mabegi ya cheda na chеnchi Yalikuwa mengi hata wachache kubeba hawaweziWalikuwepo mabinti wamefanya line up Mfano wa dinner set Sura ziko innocent Zikionyesha zina majuto ya kusign up Na baadhi yao walikuwa wadogo yaani minorsBabake Jesca alisimama kwenye chanja Ametingwa kuchanganya plama kwenye ganja Nikamsalimia hakuijibu salamu yangu Akavuta beri kisha akapiga chafya mara sabaKabla muda wake wa kumaliza Akanyonga jani akapaka mate kwenye Lizzla Akasnap vidole kuonyesha alikuwa Taita Kumwita Mrembo na mrembo akaja Na lighterMrembo akamwashia kipuri wakapiga Puff mbili Wakatoa moshi wakaanza kukiss pasi siri Ka’ wacheza ngono mbele ya Binti yake Jesca na mbele yangu kiasi nafsi ikakosa tafsiriBaba'ake aka-struggle kukumbuka jina langu Nikamwambia jina langu naitwa Toni Glove Akauliza umemjua vipi binti yangu Nikamwambia mi na jesca tumekutana kwenye coffee shopAkaisogelea glass, akanywa kilichomo kisha Aka-scan majibu Ili kuhakikisha ninachokiongea fact, akasema sikujui unatokea wapiNikamwambia nimezaliwa hapa Nonde Sua Nyumba no 77 kwa mzee Kilua.Akasema ninapiga simu mbili tatu kama hawakujui Nitakushauri tu uombe duaAkaja mtu akani-snap kwenye IPhone Design kama anafanya michongo ya passport Akainua uso nikaona umeweka ndita Akatikisa kichwa kisha akaendelea ku-type moreMkono wa jesca begani ukinipeti peti Huku moyo wangu ukienda lesi lesi Board guard wake wakinichekicheki Mara wani-search mifuko mara wani-search begiNikaletewa maji ili nipoze kiu Design hamu ilinikata mzee Wasaidizi wakingiza jina langu kwenye simu ya kimtandao Kunifanyia background checkBabake Jesca Akanipa face look kisha Akaomba simu sikubisha Akaanza kukagua photo Akalog in kwenye social kunikagua Facebook TwitterGhafla ukimya ukaitawala nyumba Wakati akili ikiwaza kufa Nikitushwa Na yale mandhari yanayofanana na nyumba ya mafia mkubwa Kutoka Kuala LumpurAkauliza je nipige down town Maana najua kila mtu kule ukinidanganya bure Nitakukausha kama kau kau mpaka uta shout shout Jesca akasema Daddy calm downMi na Tony tayari tumependana Amekuja kutoa mahari ili tuishi ka' mke na bwana Anaomba kibali anataka kunioa Na kama utakubali basi soon tutafunga ndoaBaba Jesca akaegemea kwenye kiti mwisho Akashusha pumzi kwa masikitiko Kwanini unadate na mtu hatumjui Na unajua style ya kuleta hawa wakati ringi MwikoJesca unajua hadhi ya hii business Equation ya ndoa haifiti into this case Kwanini usitafute a guy from inside Ipo time utaleta ma-spy au ma-witnessJesca akajibu daddy Tony Doctor PhD holder chuo kikuu cha oxford Anamiliki migahawa kadhaa hapa town Analipwa vizuri na kipato kinamtoshaNamfahamu Tony sio mnoko Na kwao wana uwezo sana baba yake don sio kitoto Tumejuana miaka kadhaa ameshanikaa Maana penzi nililolihifadhi moyoni sio kidogoBabake Jesca akanicheki amenuna Nikawa nimevex nimechuna Moyo unaenda resi kama duma Mabaunsa yapo next yametuna Yakisubiri mechi hii kubumaNikamwona mshikaji ameshika panga bisu Alikuwa busy anapanga vitu Sura yake ilikuwa tayari kuanza bifu Jesca akaniambia yule kaka'angu na ana anger issuesAkaja ameshika vipisi vya kete Kisha akanidadisi si kibwege Akashout naskia harufu ya polisi kwa huyu bwege Jesca akamuwahi akasema we' chizi acha usengeAkatoa syringe kwenye small bag Akauliza unapendaga cocaine Nikamwambia huwa situmii hizo zaga Kaka'angu alitumia akabwaga akajibu okayNilihisi harufu ya casket Kaka'ake Jesca alihisi mi' shushushu akani-suspect Nikahisi napokwenda sio Moyo wangu ukienda mbioBabake Jesca nae anahamaki Baada ya kugundua nina camera kwenye kifungo cha shati Akatoa bunduki nikahisi uhai wangu unaishia Ndipo polisi wenzangu wakavamia

More From This Album

More songs from this album

Join The Family

New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.

© 2026 Dizasta Vina. All Rights Reserved.