LYRICS

Search for a song or choose an album and track.

A FATHER FIGURE album cover

A FATHER FIGURE

Dizasta Vina

Waridi

A FATHER FIGURE • Dizasta Vina
Lyrics copied!
Waridi na baba yake hazikuiva Mzee alimtia hofu waliweka distance Waridi alificha yaliyonisibu kwenye kichwa Tension kubwa mfano wa maadui baada ya vitaNa alishazoea mzee kumkemea Ilikuwa adimu sana kuona baba anamchekea So, kila mzee wake aliporudi alijificha Kwani mtoto kumwogopa baba ilikuwa sifaAlipopata shida alikaa kimya alitunza Alikosa jibu alivunga Hakuwa na mtu wa kuzungumza Alisema siku…. nitakuwa mkubwa nitahama nyumbaMaswala ya shule ndio yalikuwa maongezi pekee Alipewa ada ilipofika tarehe Simu za mdingi yake ziliharibu sherehe Binti aliukosa upendo wa mzee, ilikuwa ni waziWaridi alihama nyumba kwenda kuanza chuo Akawa huru kula kunywa kuchangua nguo Ndipo akagundua milango mipya ya ulimwengu Akafurahi, walimwengu wakampa funguoAkapiga picha Dar nzima Akaijua Posta, Sinza Palestina Akajua kuna zaidi ya kupika na kufua Mzazi alimficha dunia ikamfundisha asiyojuaAkatokea Baba mwenye fedha msitu Akamjali, akawa anamsikiliza kila kitu Akamkumbatia kusema Waridi I miss you Naye akafurahi kwakuwa ana daddy issuesHuyu mzee hakumfukuza sebuleni Hakugomba alipofeli aliyofunzwa shuleni Alimwacha huru kuvaa mapambo ya mwambao Akamnunulia simu mixer bando za mtandaoAkamwacha huru baada ya nyumbani kuwa mtumwa Alimgawia sehemu ya matunda aliyoyachuma Waridi alilala bila kurushiwa stimu Mzazi alivuta waya hakupokea simuMazoea yakawa tabia, tabia ikawa hali Akampa mwili na hisia kila aliyemjali Amani ya kitu kidogo ikamvuta Hakuzuga, Waridi hadi masomo akavurugaWaridi aliruka na wazee Waridi alishazuzuka na bazee Aliukumbuka sana ule ukali wa mzee wake Alighafirika sana na hakutaka uendeleeHakurudi nyumbani wazazi walipata homa Alifata kumbatio Mwanza na Dodoma Wazee walimpa Chips Mayai na Nyama Choma Akamnunulia gari akamwambukiza ngomaMimba juu binti akageuka Single Mother Dunia ikamwonyesha Waridi jinsi ilivyo fasta Cycle ikaendelea, trauma juu ya trauma Drama juu ya drama na Depression ikam-mendeaMuunganiko wa huu upepo ukaleta tufani Sababu ya upendo mdogo alioukosa nyumbani Baba jinyoshee kidole mtoto akikosea Mpende akuheshimu akikuogopa tu amepotea

More From This Album

More songs from this album

Join The Family

New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.

© 2026 Dizasta Vina. All Rights Reserved.