–
LYRICS
–
Search for a song or choose an album and track.

JESUSTA
Dizasta Vina
Fallen angel
JESUSTA • Dizasta Vina
Lyrics copied!
Yoh.. Wanasema nilipenda bila tija, kwamba sikutaka kujifunza sikutaka tiba. Nilikupenda na mtaani ilikuwa shida. Nilikosana na watu maana nilikutaja kila midaNiligombana na wana uliposema nipunguze marafiki, ulihisi wengi wao wa nafikiria. Ukasema niache muziki, nikaacha nikatafuta kazi ilimradi nipambane na dhiki. Nikaona shega, kama kuna boya yeyote atanilaumu.....yamkini bado hajapenda. Niliitika uliponita, nilifika nikakusikiliza na kila uliponituma nilikwendaKama kupenda ilikuwa ajabu, nadhani hata ile kukonda ilikuwa sababu. Ilikuwa kufanya maamuzi si jasiri, ila kwa sababu yako wala sikujiuliza mara mbiliKisa wewe, nikabuni kila mishe. Nikapigana mpaka na kikundi ili nikuridhishe. Nilikuwa mwoga nielewe, ila nilijipa moyo kuwa chochote kinawezekana... kisa wewe. Niliamua nikupende bila 'doubt’, nilisimama kila nilipoulizwa 'nika-shout'. Sikuogopa ugonjwa wala mauti. Kwa sababu yako, nikakamatwa boda kule SauziNikukumbushe, shule nilikuwa King kwenye "dorm fights" ila nikapigwa na jamaa kwenye ’prom fight'. Mahusiano yetu yalini-cost, kuna kipindi nilikosa dili nikazama mgodiNaumwa mama, hizi shida zipo. Mama yako alipata ajali, nikatoa Figo. Nilikuwa nina mafua nakakuhitaji kama chafya ili nitoe. Nilikupenda mpaka ukanigharimu afya
Ulijua kuwa ninapenda Hip Hop lakini ikabidi nijue reggae. Sikuwa tozi lakini nikajua chepe. Nikazijua tembe. Kichwa kilipokuuma, nikazama kutafuta (ni mapenzi na sikuwa bwege)Nilijitosa kuwa usafiri, nikufikishe. Niliamua kuwa hata mwizi, nikuridhishe. Kaka zako walipanga dili ili waniue, wakaishia kuniumiza nikakanda mwiliNilikupenda peke yako, sikujua Mingo. Kuna kipindi uliniweka kwenye matatizo, kwenye vikoba ulikopa hela mpaka nikakamatwa mimi nikafungwa jela mwaka. Sikusoma, na sio kwamba nilitaka kufa na mali. Ni kwamba sikutaka uteseke ndio maana nikakupa nyumba na gari. Dili zikabuma na tarehe za kulipa zikatimia...wadeni walipokuja, nilikimbiaNilipambana sana bado nikakosa dili. Nikasafiri nikaenda kwa mganga ili niwe tajiri. Sikupenda mwenzangu ufuturu njugu, nikavuka ukuta mpaka nikaanza kumkufuru MunguNdugu walinikimbia, nakili. Nadhani walihisi zimenikimbia akili. Walidhani ilikuwa 'simple' kuniasa. Walifikia kusema nakupenda wewe kuliko 'mother'Dah! Nikavunja miiko, mpaka nikabadili dini nikawa Mkristo. Nilihadaa kufa, tulikosa mboga nikagaa gaa na upwaUlipenda kupendeza, kugeza mitindo ulipenda kuongea kiingereza. Nikakulipia shule, ulifanya madudu. Nikakubali ili usome mimi nibaki mbumbumbuNilipigana kila shari ilipokuja. Nilizuga mi ni mwalimu kwa baba'ako. Nilifulia wakaniita McMugga, na mtaani nikawa adimu kwa ajili yako"Nilitaka uwe mke", ni habari. Nilitamani nikupeleke nje ya sayari. Kuna muda nilisanda nikazama kila chaka, sikuogopa Nge ni hatariKwa yangu hiyari nikawa pusha. Nilijifanya dalali nikauza gari na nyumba. Mentali, sikungoja zali kunikuta. Mali ulipofuja zote nikaenda mbali kutafutaUlitamani rasta, nikasuka. Ulitamani shamba na duka, ulitamani khanga nikakupa. Sikuogopa nilikudaka ulipoangukaWashikaji walisema naoa lawama, nilifunga vioo tukafunga ndoa ya gharama. Kazini nikabeba pesa kwakuwa nilikuwa 'cashier’, nikakata tiketi twende ’honeymoon' Philadelphia
Sikukwambia haya yote tangu mwanzo kwa kuwa sikupenda uteseke kwa mawazo. Nilikulea ka baba’ako, sio mimi yalikuwa ni mapenzi juu yakoNilishiriki magendo, (mpaka kuua) nilitaka kuwa mjeda nikashiriki depo. Nilitamani kukuoa kiukweli ndio maana muda wote huo hatukushiriki tendoSikuibuka kilingeni, nikafunga 'decoder' na 'subwoofer’ sebuleni. Kuna kipindi nilikumbwa na madeni ili upate saluni, nikajenga nyumba ufukweniNitapunguza vipi machungu? Nilikosa nini kwa Mungu. Umekufa sikuoni tena getoniUmeniacha, Mola akulaze pema peponi. Amen
More From This Album
More songs from this album
Join The Family
New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.
© 2026 Panorama Authentik. All Rights Reserved.