LYRICS

Search for a song or choose an album and track.

JESUSTA album cover

JESUSTA

Dizasta Vina

Hatia II

JESUSTA • Dizasta Vina
Lyrics copied!
Ah! Nilipaa sasa natua Kwenye/kwenye Siri ya moyo Na siri ya moyo Anayeijua mwenye/ Mwenye ujasiri wa Kutunza nafanya Ninachodhani ni Sahihi kitachotokea Nitajua mbeleWanasema mwanaharamu Haijui laana/ kashalaanika Nasikitika kuwa haujui Kama/ naonekana ka' Kondoo kwa mchungaji Lakini...lakini kwa ndani Mi’ ni chui mamaKwa mfano nakuita mpenzi/ Na tabasamu zuri wakati Najua kuwa sikupendi/ Kuitoa hii siri ndo' siwezi/ Kwahiyo nitakudanganya Mpaka ifike siku niutimize UshenziHuwa nawaza nikuweke Ufahamu/ mtambue Kuwa mpo wengi Na lengo niwateke Kwa zamu/ niwaumize Ili mpeleke salamu/ Masikini mrembo Nashangaa jinsi unavo'ngoja Pete kwa hamuVile hunioni kwenye Makundi ya baa/ Na bahati nzuri haujawahi Kusikia nikizushiwa uzushi Kitaa/ nakununulia Rubi kadhaa/ unahisi nakujali Kumbe unampigia mbuzi gitaaSometimes unanisongea nguna/ Au wali ukidhani mi’ najali ilihali Sina habari, sina hisia siwazi Hata kukuonea huruma/ Na sibadili dhambi hata Mbingu ikisogea nyumaAh! Nashiriki nawe nyakati Twitter mpaka instagram/ Picha unani-hashtag drunk in love/ Nanunua brand za gharama za Hand bag/ perfume kali Simu ya ghali breakfast Zanzibar/Haimaanishi kuwa Tunaianza safari/ Nataka nikuandalie maumivu Makali/ nahitaji nikuguse Ili kila unachokiona Kiwe kinafanya unikumbuke Ni hatariInaitwa zuia nanga kabla Bado haijang'oa/ Maana haujaheshimu Mvua kama bado hujaloa/ Kwa huu mchango ninaotoa/ Ndo' unafanya unazama Zaidi kiasi unaiwaza mipango Ya ndoaJicho la tatu hauna Fungua jicho lako la pili/ Utagundua kila ninachofanya Kwako batili/ unanipenda mno Ndo' maana haujaona bado Dalili/ kuwa we sio wa kwanza Wala haupo kwenye Mpango wa pili Ah!!Unaniletea zawadi toka Majuu/ kuna wenzio Nilishawaacha Na walinichora tattoo/ Mi sio tunda mama... Mama mi' kidonda Utachelewa kusonga Ka' bado unaingoja nafuuSherehe ya birthday yako Kwenye 'temple' ya anasa/ Umekuwa ’mental’ kwa Huu mwendo ndo' Umenasa/ Kiasi unahisi huu ni upendo Na sasa/ hautambui kuwa Tukishiriki tendo tu nakuachaKichwa changu hichi,kichwa Changu kishajadili/ kwamba Nitalala na wewe na Wewe na haifiki jumapili/ Nitakuwa nimeshakuacha Ah! utanitafuta Kwenye simu ambayo Namba nitakuwa nishaibadiliUtanitafuta mara mbili/ Mara tatu kisha nne Utagundua kurudi Sina dalili/ ngoja ngoja Itang’ata moyo wako Kikatili/ mja wa Watu maumivu Hukujiandaa kuyakabiliUtanipamba majina ya Kikafili/ sitasikia maana Nitakuwa mbali nishasafiri/ Nishasahau utatunga nahau Kukanda mwili/ na huo Wakati haukuwahi kuutabiri/ Ila upoUtaumia utashindwa kusimulia/ Utaniulizia kwa wanaonijua Watakwambia/ kwamba Hauna tena chako Okota vipande vya moyo wako Nenda zako kaandike TanziaKisha watajua wenzio/ Wanafiki watacheka Wanaokujali wataangua kilio/ Watakusindikiza kulia/ Watakupa pole wengine watasema Tulikuambia/ kuwa Wanaume wote mbwa!!Taswira itazongwa Na wingu/ Picha utazichoma Kwa kisu/ Utanitukana mara mwana Haramu mara malaya/ Rafiki zako wakuu watakuwa Filamu na riwayaWimbo niliokuimbia Kamwe hautokukonga/ Utachoma mkuki moyoni Kisha kunyonga/ Utaendelea kungoja/ Utagundua mvumilivu Hali mbivu hiyo Methali iliongopa/ Utagundua ilikuwa Ni soga/Hii itafanya ukonde Na kuanza/ Kutumia pombe na ganja/ Nayajua haya yote Kwa maana ndo nilikotoka/ Utasimama kijasiri Na mwisho utadondoka/ 'sikiliza'Wataleta daktari Akuulize nini shida/ Hawatapata Jawabu kabisa/ Wataleta sheikh Wataleta mchungaji Wa kanisa/ Watasahau kwamba Moyo uliovunjika Hauna tibaNatamani nikuambie kuwa nimekuteka makusudi/ Maana unasikia na hujifunzi/ Nikuumize kama mke wangu mpuuzi/ aliyekimbia na rafiki yangu siku moja baada ya harusiNilishaambiwa na Mama nikapuuzia/ Kuwa haujawahi Kupenda kama Haujawahi kulia/ Kuna muda mtu mbaya Hutengwa na hatia/ Maana kafiri hazaliwi Utengenezwa na duniaUkijiua sitakuona Mzembe amini/ Nitakuvalisha pete Ruksa uipeleke baharini/ Najua tiba ya Upweke amini/ Mwisho wako ni Kuwa kicheche kama MimiHapo utajua kunihukumu Sio haki/ Mwanamke kama Wewe ndio amenifanya Niwe muasi/ Bila hofu wala Kiwewe/ Nitaendelea kuzunguka Kutafuta wasichana Vipofu kama weweSina hatia ..

More From This Album

More songs from this album

Join The Family

New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.

© 2026 Panorama Authentik. All Rights Reserved.