LYRICS

Search for a song or choose an album and track.

JESUSTA album cover

JESUSTA

Dizasta Vina

Hatia III

JESUSTA • Dizasta Vina
Lyrics copied!
Ah... Nakusalimu mwafrika...nakusalimu habari gani.../ Nikaribishe tuketi...niseme yaliyo ndani.../ Sahau kuhusu hadithi za kale...za upendo wako.../ Nataka leo tukae...tuijadili kesho yako.../Kutoka kupiga ramli...na kutii mizimu.../ Umeanza kufata amri...za TV na simu.../ Na ubaya ni kwamba...umeanza kuikacha sanaa.../ Na kufata siasa...ambayo inakulaza na njaa.../Na kila unachokiona...unataka kubeba.../ Vichache vimekushinda...na unapanga kuongeza.../ Juzuu,Katekisimu mpaka Novena.../ Sio zako...zako zilikuwa ni kutamba ngojera.../Umezubaa...majirani wameanza kufika kwako.../ Na unaamini kuwa...watakubebea shida zako.../ Kwa sababu ya ujinga,umezidi umasikini.../ Unamjengea jirani...kwako unachimba unabaki chini.../Zamani...ulikuwa una sembe ya kusaza.../ Uliabudu kazi...ukaliweka jembe kwenye shamba.../ Ghafla ukauza panga...ukapamba jembe kwenye kabati.../ Ukanunua kioo ujirembe...ili uende na wakati.../Ume...chagua urembo na umetupa werevu.../ Umeuza mifugo...unafuga kucha na ndevu.../ Familia iwe...mwafrika uzame mitini.../ Au uombe msaada..wakati unakufa na fasheni mwilini.../Mwafrika..una mzigo mkubwa wa madeni.../ Hauna mali ..ardhi yako ni 'future ya wageni.../ Unalala ndani...kungoja hisani ya wenye nguvu.../ Nyumba iko wazi..wewe uko ibadani unaabudu.../Ujasili ni kujimudu...mwafrika haujui hili.../ Umejaliwa nguvu...na unashindwa kuzihimili.../ Unavamia diplomasia..unatunga hotuba.../ Na hakuna mwenye hisia...kuwa upo nyuma ya muda.../Ah.. Unapoteza stadi za maisha.../ Kwa elimu ya magharibi...ikuweke ofisini suti kubwa.. Ukumbatie dawati la nyazifa.../ Huku unauwa..nguvu kazi ya taifa.../Umepitiliza nyumbani...hauna vituo.../ Umekuwa mtumwa wa sera zao,kiasi kwamba hauna 'future.. Hauna dira,hauna lugha hauna nguo.../ Milango ya fahamu..imefungwa na ufunguo.../Umepewa karatasi...ukaita jina pesa.../ Ukasubiri ikuletee furaha..ikakutesa.../ Ukauza umoja...ukauza amani ukauza utu.../ Ukawashusha mashujaa wako..ukamwinua Yesu wa kizungu.../Una kucha ndefu ..kushika chungu matusi.../ Hauwezi kuandika history..haumudu herufi.../ Ume-bleech nywele,mdomo mwekundu umebusu baruti.../ Nikuite nani...mwafrika mzungu au mzungu mweusi.../Ah.. Unadanganywa...rangi yako sio nzuri.../ Ili utafute pesa...ukawaungishe vipuri.../ Ume-switch kutoka Mama Afrika...mpaka drama Queen.../ Una nunua TV...uone Afrika ikizama chini...!/Mwafrika..umeshakosa mipango.../ Unajua kuchonga ngenga..badala ya kuchonga vinyago.../ Unaacha wanyama Mikumi,Serengeti unasafiri.. unaenda kushangaa ghorofa Chicago.../Unarudi..unajikuta Mmarekani eti real nigga...!/ Mbona haulili bili nigga...?/ Jasiri..haiachi asili real nigga.../ Kamwe usijiite G nigga.../Hauwezi kuwa warrior../ Unajua majina ya wasanii..kishinda historia.../ Unasahu mapishi..hauendi jikoni.../ Unakufa na ngoma mwilini...cheni shingoni.../Kwa heshima na taadhima...unautunza Msaafu.../ Unatupa kitenge..kisha unafunga hijabu.../ Na ubaya ni kwamba...bado haujajua sababu.../ Unapewa Zaburi..utafakari mwenyewe wakichukua dhahabu.../Ufeli majibu...uishie kubuni.../ Ushindane nani msafi...aende mbinguni.../ Mhanga wewe...rudi uzipitie kanuni.../ Umeshikishwa kitabu...wenzio wakushikie uchumi.../Mwafrika...hii haikuingii nikichana.../ Unanuka sana...kiasi hauvutii kama Jana.../ Kiburi moyoni..haisikii unapokanywa.../ Unatia aibu..kiukweli sijivunii kuwa mwana.../Na bado unaamini..shahada ya shule ni zana.../ Haujui...ukitaka ule ni shamba.../ Unafunga ubongo...unafungua mikono ili wakupe msaada.../ Umesahau kuwa...vya bure gharama.../Mchezo wako...sheria zao utashindwa.../ Ukiishi porini..kama haiwindi..utawindwa.../ Inasikitisha..wenzako wanaigiza ili waishi...ila we unaishi kwa kuigiza sio...?/Umekuwa dekio..umekubali kuwa soko la pombe Na sigara.../ Soko la risasi bunduki na mabomu... Soko la madawa ya kulevya..yanauwa waafrika wenzio.../Soko LA dini zao..soko la picha za uchi .../ Soko la vitukukuziba sauti.../ Soko la sera unevu..na mifumo gombanishi... Magonjwa batiri..unanunua dawa kwa kuhisi sio...?/ Umezagaa visingizio.../ Haujui akiba..ndio maana unashangaa salio.../Umegeuzwa kifaa cha majaribio.../ Imeandikwa..asiyeandaa silaha ataandaa mapambio.../ Mwafrika...Nakupa nahau kalili.../ Afrika inakufa..mwafrika unadharau dalili.../ Unasahau wito..unafata mkumbo kwa dau batili.../ Unakumbuka kila kitu..na unasahau asili...

More From This Album

More songs from this album

Join The Family

New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.

© 2026 Panorama Authentik. All Rights Reserved.