LYRICS

Search for a song or choose an album and track.

JESUSTA album cover

JESUSTA

Dizasta Vina

Hatia

JESUSTA • Dizasta Vina
Lyrics copied!
Ah.! Niambie ilianza vipi najua haikuanza ghafla Zipi dalili maana hata mafua huanza na chafya Kivipi mi kaka'ako na ulisita kuniambia ukafanya siri ina maana kimsingi nawe ulitakaAh! Kimsingi nawe ulitaka kumbuka Tangu baba mzee Muggo anakufa Alituusia uaminifu na ndio nguzo uliyoiangusha Nashangaa bado nafsi yako hijasutaMaana bado natamani kukujali Mdogo wangu natamani sana lakini imani yangu imekufa tayari Sometimes nakwenda mbali Natamani kukudhuru busara inaniweka huru nagundua mi sio mshariUlianza vipi kumtamani wife Je ni siku namwoa? Au ulianza kabla ya siku ya ndoa Na ndio maana siku ya harusi ushirikiano ilikuwa ni ishu kutoa Kama harusi ni pingu nang'oaSihitaji tena Najiuliza kwanini nilibashiri Lakini nikapuuzia dalili Kwanini nili..... Ah It all makes sense nowSubiri mwanaizaya subiri it all makes sense now Mwezi wa pili hanipi penzi now Yaani kipindi nashusha pensi down Ananiambia kuwa amechoka anahisi kama homa hawezi... How??(nimiminie wisky) Sikujua kuwaacha pamoja home ilikuwa ni risky That's why I've been away for so long and she never missed meSikiza... Sijui unachofikiri rohoni bado Maana upo kimya niseme huoni mwisho huoni mwanzo Ulikataa kusoma chuoni ng'ambo Ubaki ule ninapokula kweli kikulacho ki nguoni mwakoTulisimama kama mdogo na kaka umeng'oa nguzo Hongera kwakuwa Mpumbavu yanipasa kutoa tuzo Have you started using cannabis?? Man i thought we are brothers I thought we are bond now we are enemies Enemies...Hii maradufu imeniumiza Acha uliponiangushia mninga Au ulipogusa mzinga nikakuokoa Upole ulizidi ukaniona mjinga Ukaamua kumshika sharubu simbaAh! Remember we use to build a snowman Go school together playing ball and I can't believe that my own brother sheg my own wife on my own bed ( On my own bed..)Nilitaka tuwe saresare Ningaefadhiri mbuzi ningekuacha uwe palepale Mabinti hawaishi ukianza huwamalizi ukasahau visima vingi ila maji ni yaleyaleTulikuwa kama mwiko na wali Ulikuwa kijana mzuri mdogo nakuvusha kijito cha maji Umebadilika umepoteza nguvu na ufanisi Mtaa mzima unatembeza rungu kama mlinziNilijitoa sadaka ili ufike far Maana sikutaka ikufike njaa Hukutaka unisikilize na Ukachagua kuvunja moyo wangu vipande i don't even know where the other pieces areVile Niliamua kukulea Ah nikakulea kama yai kama... Ukaamua kunioneaKaa kimya.. Kaa kimya ngoja nibonge We ni mdogo wangu toka nitoke Inaniumiza sikukwambia tangu mwanzo kwamba huu mwaka wa tatu mi na wife... Tunagonga vidongeOh men she killed you That devil killed you Labda nimeekuua mwenyewe labda ningekuambia kuwa.. Kuwa sisi ni waathirika ila nikasita.... Men I'm still a foolYes I'm still a fool..Nikiandika overall summary Nimekuwa mjinga 'cause i killed my own family(Nimekuwa mjinga 'cause I killed my own family...)Kwakuwa nimekulea nimewajibika Umesoma umepata kazi ya kuheshimika Nahisi kama kazi yangu imekwisha nimemaliza, naondoka naenda mbali maana kuwaona inaniumizaZingatieni tiba...(Zingatieni tiba...)(Zingatieni tiba....)Kumbuka kuugua sio kufa.. Niahidi hautajuta..Kwaheri

More From This Album

More songs from this album

Join The Family

New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.

© 2026 Panorama Authentik. All Rights Reserved.