LYRICS

Search for a song or choose an album and track.

JESUSTA album cover

JESUSTA

Dizasta Vina

The Lost One

JESUSTA • Dizasta Vina
Lyrics copied!
Alivaa sketi inayoangaza ilikuwa nyepesi Fupi unaweza dhani ni kidenti Japo nilikuwa single ila sikuwa mingle Alizidisha maringo alipogundua namchekiHaiba ya aibu mfumo wa kibinti Kidogo rangi na lile umbo la kimisi Akiweka pozi nihakiki Alikuwa anang'aa ila ngozi yake ilisanifu dhikiBado ilikuwa hainiboi kumtazama Macho yangu yalikuwa yana-enjoy alichofanya Kiasili nilikuwa hoi kiasi cha kutogundua alikuwa na konvoi la mimamaKwa mtindo wa kujongea kwa madaha Yule malaika akaanza kusogea nilipokaa Hata kabla sijaamua kumchunguza Macho yaligundua kuwa binti anajiuzaHiyo iliweka ufa moyoni Nilitamani hata kustuka ndotoni Kwakuwa nilipata hisia kali za upendo Nikawa tayari hata kujitupa motoniNilitekwa i only needed her for the rescue That's how far love can take you Nikataka mpaka kumvika pete Awe mchumba nikasahau mwenzangu anawaza cash tuNi aina ya wasichana wanaotokea kwenye ndoto Yaani unafumba macho alafu unaona anakulelea watoto Kwa mara ya kwanza maishani mwangu niliwaza ndoa Hasa baada ya mapenzi ya wasichana wa town kuniboaAkiongozana na kundi la wenzake Akasogea akitoa sauti za kipambe Kila mmoja akijinadi kwa mikogo ya mahaba Nakumbuka mmoja alivua brauzi nimtomaseAlijinadi kama ng'ombe mnadani Nikataka nijitose chakani Yaani nijitoe sadaka nilimwona kama kidani cha dhahabu Maisha ya mjini yalifanya ajione hana thamani Tukagonganisha macho kihisia Ndio nikajua nimezama na sijui nitakapoishia Apendae kipofu nikazisahau kasoro Nikashuka nikamfungulia mlango akaingiaKwa pupa nikadrive mpaka home Nilipofika hata kuzima gari sikukumbuka Kuna muda nilimkuta uchi kitandani Anauliza kama tunaenda kavu au kwa ndomNikamsihi avae nguo Akahamaki akauliza maswali mawili kwa mkupuo Jogoo hawiki braza au ume-mix machaguo Nikamjibu mi msafiri na wewe binti ndio kituoKwa jicho la kufuga kisasi Akanicheki kiasi kwamba niliyumba kinafsi Akanikumbusha hajaja kwangu kutafuta hifadhi Anafanya biashara na kwangu amekuja kikaziNikashika usemi uchafu ukiingia kwenye kapu toa Usitupe kapu kwahiyo sikumwona kama changudoa Nikamwambia nikimwangalia Kwanza nawaza kujenga pili familia na tatu ndoaHakuitikia akanitenga na himaya ya majibu Moyo wake haufunguki na ninahitaji rai Hatukuwa sawa nilitaka kujaribu Akanijibu Kipepeo na nyuki hawatagi yaiAkaniruhusu kumkumbatia Akashika mikono yangu akaibusu kwa hisia Sijui alinipa nini nilijikuta naanguka Kizunguzungu ile kustuka kumekuchaNiliamka na mawenge kichwani Nilighafirika kugundua hakwepo chumbani Aliondoka aliniacha na aibu mtaani Maana aliposepa alibeba kila kitu ndaniAlikuwa kunguru na nilisahau hafugiki Hata iwe kibudu kwa nyanya na limao haungiki Alibeba vipi sijui kinachoniuma Ni kukosa pendo la huyu bintiSitasahau macho yake mawili ya kirembo Sauti iliyowasilisha upendo Akipigwa vikali na ubatili wa matendo Ya mwili wake mzuri ambao haustahili matesoAliniachia meseji alipoondoka Akinipa pongezi kwamba sikuwa mwoga Kuufuata moyo wangu akaniomba msamaha Akisema hawezi kuenzi penzi ambalo kwa wazazi alikosaSawa ah! Nimekusamehe zamani mami Pendo lako dawa ewe baniani Niahidi utawasamehe wazazi wako pia Ambao wamefanya uonekane shetani honeyI'm kinda lost I do things i ain't suppose to I thought you'll be my best friend that I can talk to I wanna change if you wanna change I'll support you I think we both need the way out that we can walk throughAh popote ulipo ambapo info inafika Bado mrume nipo miaka inapita nauandika Huu wimbo umenifundisha nisitue mzigo kama ninahisi sijafikaNaoa kesho na nina hamu kukukuta Nikwambie dunia safi binadamu ndio uchafuka Ni kawaida usisahau kutabasamu kukikucha Nakuombea afya kwenye nyama damu na mifupa

More From This Album

More songs from this album

Join The Family

New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.

© 2026 Panorama Authentik. All Rights Reserved.