LYRICS
Search for a song or choose an album and track.

NDUGU WA MBALI
Dizasta Vina x Kaa La Moto
Shaaban na Ngugi
NDUGU WA MBALI • Dizasta Vina x Kaa La Moto
Lyrics copied!
VERSE I — DIZASTA VINAUjio wa kasi na hadhi ya makombora
Kichwa cha kazi, kadhi ya Hifadhi ya tungo bora
Jihadi ya kutochoka, hitaji ya tunzo chora
Kuona tofauti kati ya miradi hii ya WakoraNa baraka za mababu, sauti inaongea
Kwa mahesabu ya dhahabu, ni aghalabu kukosea
Ajabu ya hii rahabu, si upatu wa kuotea
Na katu sioni tabu hizi tanzu kuzichocheaIlani zina rehema
Wachawi wa miji yote ya mbali na ya jirani, imani zinatetema
Ghani zinawiwa vyema, zinachapishwa tenzi za ndani
Unaweza ukadhani Shaabani kazaliwa tenaMswahili, uhali gani? Ihali gani kani?
Ya msukumo wa kujifunza kutunza ilani kali
Ya masimulizi na upangaji wa silabi nami
Nakusafirisha hadi uhisi nyumbani mbaliHuu ujio ni ishara ya tanzu za maana
Kwenye vitivo vya mijadala, sauti yangu ni gharama
Nikizuru mihadhara, wanga wanachagama
Usiende pao pakavu na pangu pana salamaDarasa linamdadisi mwalimu
Linataja na jina ili kuonyesha linasadiki hizi mbinu
Kichwa hiki sio kinu
Nabusu ardhi kushukuru asili iliyoumba kipawa hiki adhimuMidondoko ya tungo adimu
Sentensi zenye misimamo, unaweza sema nyundo ya hakimu
Naganga mbele, sisikii jeuri za wadhalimu
Napanga herufi na herufi zinaleta tarakimuKwenye hundi
Jarada la makada wanasema mi ni fundi
Wanajipanga na wanasanda kwa makundi
Hakuna msaada wa majani au gamba kichwaniHakuna uchawi, ni ujuvi na ulumbi
Kwenye vituo vya sakarani, mi ni mbuji
Misamiati hapa imelala kwa mkufunzi
Gharama gani kwenye chakula, ila wakatiWa mapishi tunajua chenye thamani huwa ni chumviJumbe zinasafiri ka fununu
Tunu ya sentensi ya kikatili ka hukumu
Sumu wanajadili, ka kutano la siri
Mawakili wanakesha kunikabili ka jukumuStanza zinapangwa kwa vitaru-vitaru
Kwa waja wateketeke na vijana barubaru
Akili za waruwaru zilishindwa, ni patatifuNyayo zangu zikigusa marumaru
Ahh, nimesheheni silaha kama manowari
Kila msamiati una uzito wa matofari
Ukiona utofauti wa kung’aa na umaridadiTambua mi sio mwenzako, damu yangu samawati
Kazi yangu ni harakati, mistari ni sala safi
Wabanangaji wote ni mfano wa karimati
Ukubwa na ujazo ni mafuta-mafutaUkigusa, ukigusa, utakuta pana hewa katikati
Koja la lugha sahihi linakaangiza
Fasihi inaimarishwa, utabiri unakamilika
Jamii inafundishwa, unabii unakamilishwaHata walobisha wote wanatii, kwa hakika
Ukiniona kwenye rununu, penda
Fununu zinasambazwa kuwa mimi ni ndio tunu ya malenga
Kazi ya kuchochea sukununu na tafitiKufikiri kwa uhuru, huru kwa walengwa
Sina wema, ila sio mhuni kwa matendo
Kama lulu natafutwa na Warumi wa Efeso
Naheshimika na wachumi wa MasakiNasikilizwa na walala hoi wa Buguruni mpaka Keko
Salamu wachimbaji, hiki kitalu sahihi
Unashikishwa adabu na manju mahiri
Anayepambana kuufuta upumbavu wa jijiNa kuleta habari njema ndio yangu nadhiri
TwendeVERSE II — KAA LA MOTOHii kalamu ipo huru, nawakata-kata, Kalima
Kwa hii fasii ilojaa nuru, Allah, Rasulu, Madina
Nashukuru kwa hii zawadi, sitoikufuru, Karima
Amini yeye ndiye mpaji, kanipa kipaji, NgirimaKuna siku nitasimamiwa, watu hawatashuka, sijida
Acha nifanye leo, hata kesho nikishuka, siji Dar
Mtanikumbuka kama mwanazuoni, Nassor Bacho
Na sioni wa kunisimamisha, hata kwa mpako wa SabatoMi waziri wa madini kama sultani, Ali Hassani
Zanzibari kama Mwinyi, niwekeeni siti yangu Pwani
Nguli kama Siti, ongeza tashtiti kuhusu kijiti
Au iongeza misamiati, tumbiri kaiona miti?Tafsiri hii, mdomo ni mmoja, masikio mawili
Na taarifa ni za mauaji, na vina watazika mwili
Kwa kina watajadili, kisha vunda hakina ubani
Wakina fulani hawachezi na sisi, tuna roohaniHiki kichwa kimeshinda masheikh na makuhani
Malbadiri, majuzuu, marukia na mayasin
Bei zimepanda na siuzwi reja-reja
Mpaka TMK, wazee wa mapanga, njooni mmoja-mmojaUsinichukulie poa, ama wa ziada tu kama Rashid
Nitakukamua, njoo kichwa-kichwa, kula za uso saba
Kwa game tumevaa mabomu, kama tunakufa shahidi
Niliona bora kuliko ngada ama kuanza kukabaShahada za uzamivu ya heshima, honoris causa
Ukiniona kausha, huku unapigika, hata uwe baunsa
Mali ka Mansa Musa, tap, maji yanakauka
Navuka upande wa pili, halafu namuachia JoshuaBaada ya hii tunaacha alama, niite Tetekuwanga
Na bado nina ufalme wangu, na sijabaka Buganda
Labda Daudi, kwa PAC hii, nashusha mabigi
Goliathi ama King Saul, nakuwa mfalme wa WayahudiMi jabali ka Mwanza, zinasifika Faridi
Nilipomzika Qubanda, na nikalijua na jiji
Kama Eskimo, sioni wa kunitia ubaridi
Hiki kipaji maridadi, mix ya Shaban na NgugiChunga sana ukiambiwa una future na watu wako nyuma
Hawaharakishi,watakukalisha ka sumo na Yokozuna
Hiki chumba cha upasuaji, tunakosa huruma
Kuua marapa ni faradhi, kuwazidi tenzi ni sunnahRapa toka enzi, game halina ushenzi wala Macheda
Halina hifadhi, tuzo ya malaika anapewa Makeba
Tuna mali, usisahau zawadi alitoa Makeda
Saiz zinaumia nyeti, tukiacha madogo washike begaZinapotea vyeti, ukisikiza beti kwa hawa wajuba
Kiswahili na fasihi, nahau kama nipo Unguja
Nawachenga na lugha, nawavuruga waliokuja
Hadi wanasahau kuwa mi ni mbora wa kila mudaNa sijazeeka bado, nipo gado, usilete uchuda
Na ikitokea nimekufa, zibaki hadithi na ushuhuda
Bado aluta inaendelea baada ya Kaluta, Amir Abedi
Na Saadan Kandoro ama Muyaka bin HajjiSijui imekuaje, wachenguaji wamekuwa wachekeshaji
Na kule kwengine, mchekeshaji amegeuka mcheguaji
Ni kazi kubwa kama kuishi na samaki nje ya maji
Na tusipochunga, vipofu watageuka watazamajiHe baba, tupe hifadhi, kalamu zinaisha wino
Tunakosa mahujaji na elimu ya mtaani ka D Knob
Wengi wanakata viuno, usininukuu vibaya Chino
Kwa kuwa nyie ni singers, cherehani kuna mishonoTungo zina flip-flap nyingi, Rivellino
Unaweza zig-zag ama keep it straight, Gogo Simo
No elastico, first kwenye list, last siko
Naandika ninachokipenda, maandiko, Steven BikoHatupo kwenye sakata, nani mbora kuliko huyu?
Tunaishia kujitukusa badala ya kutukusa Mbuyu
Kusudi ni moja, azma ni moja, kufikia nduyu
Kupata mapene, usije kuhurumisha ukifika MbuyuTangu maa, baa na irabu, toka vidudu
Mpaka maabara, semi na tenzi, zote namudu
Niko too proud kwa hii kitu, naifanya kama sugu
Level za Ki-Taita, kabla sijakua, chakula cha waduduWatunzi wananiogopa, nitatoa siri kama dudu
Na sio juu ya pombe, zinatunzwa asili kama juju
Chini zimelala diamond, juu daymond kama Fubu
Jini huria, mi ni adili, naomba uwasamehe nduguHaya, mnikome mfugaji, zizini mbuzi hatushindani
Hapa kazi juu ya kazi, mjomba, hatushindi ndani
Na uwaambie watoto wadogo pia, hatuishii ndani
Nawapa joto, hata kama sote tuna-share faniNimekuwa classic toka minor, kageni kwa mchezo
Kwa haya maelezo, sioni wa kunizidi kwa mchezo
Juu kileleni, so keleleni, zimelala Kibo
Napaa juu uhuru, si kaa tai juu, egoNashukuru nilichonacho, na pia nashukuru ambacho sina
Najua nitaipata kesho, cha muhimu leo nipo mzima
Kama uliskia wanatema, jua sio tamu yao
Ama amesifiwa mgema, sasa wamelitia maji tembo lao
More From This Album
More songs from this album
Join The Family
New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.
© 2026 Dizasta Vina. All Rights Reserved.