LYRICS

Search for a song or choose an album and track.

THE VERTELLER album cover

THE VERTELLER

Dizasta Vina

A Confession of a Mad Philosopher (feat. Dash)

THE VERTELLER • Dizasta Vina
Lyrics copied!
Maana ya uhuru huisha baada ya utambuzi Baada ya kutambua kwamba uhuru si maamuzi Maana Kifungo na mipaka vinafanana Aliyekuambia kuna uhuru utaupata kakudanganyaIpo asili inayofanya mwili wako mashine Kufanya Ugonjwa uwe jela alafu afya ni jela nyingine Mjamaa amemwaga damu tayari Awe huru ili akawe mtumwa kwa mabepariChagua kufa ukiona waja hawalipi wema Kufa wokovu kilichokufa hakifi tena Kufa ni uhuru kamili tabu ni nini Haupo huru sasa uhuru wa kweli ni kaburiniUnakumbatia uhuru wa kuambiwa Wakati unaishi na haukuchagua kuzaliwa Uhuru hautafutwi msafiri pumzika kubali chai Hauwezi kuwa huru ungali haiUhuru si halisi jamaa badili umbo Uhuru sio jibu hata usikariri fumbo Uhuru ni falsafa ya vitabu iliandikwa na mababu Tutaisoma na mwisho itabaki hukoAnayehitaji uhuru aelewe Kuogopa kufa ni utumwa kwa maana kufa ndio uhuru wenyewe Hata uwe mfalme ambaye anatoa idhini Huwei kuwa huru uhuru wa kweli ni kaburiniFreedom freedom Freedom freedom Freedom freedom Freedom freedomUkikumbatia mwanga jua utaificha nuru Uhuru si kwa mwafrika kumkimbiza mkabulu Kuutaka uhuru sana jamaa si dalili njema Kama upo hai na unahisi uko huru fikiri tenaCheo huleta nuru pahala nuru haifiki Na pesa ndio njia ya uhuru ukiimiliki Pesa na cheo upita kule hakuingiliki Alisema mlevi mmoja ambaye pombe tu imemdhibitiMwathirika ambaye dawa za kulevya zimefunga Na anahisi yuko huru mara baada tu ya kuvuta Labda si kweli haupo huru ukijiongeza Maana ukishaujua uhuru tayari ushaupotezaJe utaniona chizi au mwivi Au pumbavu au mshenzi ninayeongea vituko Au utaamua ukae chini utafakari Kisha ukakubali ndoa ajira navyo pia vifungoAliye huru ni nani nieleze mtoto anayeenda kwa viboko Au mlokole mtenda mema baada ya kutishiwa moto Au msomi elimu mpaka chuo kuhakiki I swear kama uhuru ndio huo siuafikiAnayehisi yuko huru pita mbele Piga kelele maana hata Mungu wako hayuko huru Hawezi kubadili mipango hawezi kumuumba Mungu mwingine mkubwa kupita yeyeUnaetafuta uhuru wa kweli utateseka Utapoteza damu utatoa machozi na utakesha Hauwezi kuupata maana hakuna ulipouweka Uhuru haupatikani kwa fedhaUhuru is priceless kwakuwa si bidhaa halisi Wenye chapaa walihakiki Utaniangusha sana ukishindwa kuamini Upo uhuru ila uhuru wa kweli ni kaburiniYou've got no freedom You've got no freedom You've got no freedom You've got no freedomFreedom freedom Freedom freedom Freedom freedom Freedom freedom

More From This Album

More songs from this album

Join The Family

New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.

© 2026 Panorama Authentik. All Rights Reserved.