LYRICS

Search for a song or choose an album and track.

THE VERTELLER album cover

THE VERTELLER

Dizasta Vina

Kesho

THE VERTELLER • Dizasta Vina
Lyrics copied!
OkayWanasema tomorrow is the mystery Wanasema tomorrow... Leo zawadi ikumbatie, jana ni History Ya jana hayawezi yakafana kwenye script hiiWanasema tomorrow is the mystery Wanasema tomorrow... Leo zawadi ikumbatie, jana ni History Ya jana hayawezi yaka....Ah Kesho nafasi ya kuanza upya Kumaliza kuishi nafasi ya kuanza kufa Kuivunja sheria nafasi ya kufata ruksa Kuikumbuka jana au kuanza kuifuata FUTUREFUTURE ni leo siku ambayo miti hukimbia Jua hushuka upendo wa marafiki HUFIFIA HUFIFIA wimbi la wanafiki huingia Kesho ya TUMAINI hubakiaTUMAINI shika walau shika walau Na ujifunza kuziba kombe pindi anapopita nyang'au Akishapita tenda wema alafu kisha sahau Na uchunge unaponena watakuzika WADAUWADAU walikuwa uchi ukawavika mavazi Nyumba yako ikavunjika wakakunyima hifadhi Je utasamehe utasahu kulipa kisasi? Au kesho itakukuta umeshika RISASI?RISASI nawaza wapi itakukutisa kesho Utatoroka kambi ama utavungia Ghetto Tusipofikia lengo utahama ukoo kwa kitu kidogo Au utaiitumikia NEMBO?NEMBO ya mjeshi ninayekaza mwendo kishujaa Kama unavyoza nyonga kwenye tendo la zinaa Napiga goti nashukuru uwepo wa sanaa Kihisia nawapelеka kesho MAJAMAAMAJAMAA walikuwa wavivu hawakukazana Waliishia kuamini kuwa kuna wingu la laana Wali-set mipango ila siku hazikufanana Huwezi kuikabili kеsho kwa mbinu za jana ah!Wanasema tomorrow is the mystery Wanasema tomorrow Leo zawadi ikumbatie, jana ni History Ya jana hayawezi yakafana kwenye script hiiWanasema tomorrow is the mystery Wanasema tomorrow... Leo zawadi ikumbatie, jana ni History Ya jana hayawezi yakafana kwenye script hiiNakuwekea Logic penye Faith Nakutazama ukishahama nakuwekea topic kai-debate Ninakunyima msosi kwenye Plate Njaa ya kesho ikufunze kuheshimu pochi yenye PAYPAY huna unatia neno kwenye bao Ukirudi unalalama kuhusu kesho ya wanao Myahudi ukisujudu kwenye uwepo wa Farao kwa wayahudi Utaishia kwenye Tempo ya KARAOKARAO kazikwa kama Historia ilivyozikwa na jana Kesho ni siku ya kujitwika lawama Kesho ni mbali natumai nitafika salama Najipa moyo kisha ninaibusu picha ya MAMAMAMA sishiki simu wakati na-drive sitii vocha Na mafuta full tank kwa gari sisikii uwoga Big G za kutosha, Chupa za maji na Diclopa Na Cd za muziki wa Papii KOCHAKOCHA kasema Kesho inataka bidii tosha Nawaeleza watu wangu na bado hawasikii hoja Wamesahau kesho ni nini, Niliwaamini leo najuta Ila kesho sirudii KOSAKOSA ni kuchoka maana akili haifikiri Taswira ya kesho naiona na mboni hazihimili Kelele zimeshamiri masikio yameshagota na Na mdomo unaropoka, Dunia haina SIRISIRI ikasambaa viganja vikanakiri Miguu ikalemaa ila ubongo ulikariri Tumbo halikujaa na mwili haukunawiei Kesho ifike mapema inikute nipo KamiliWanasema tomorrow is the mystery Wanasema tomorrow Leo zawadi ikumbatie, jana ni History Ya jana hayawezi yakafana kwenye script hii

More From This Album

More songs from this album

Join The Family

New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.

© 2026 Panorama Authentik. All Rights Reserved.