LYRICS

Search for a song or choose an album and track.

THE VERTELLER album cover

THE VERTELLER

Dizasta Vina

Kibabu Na Binti

THE VERTELLER • Dizasta Vina
Lyrics copied!
Mhoji: “Mmhh… kwahiyo ni nini kilikujia akilini aah!! mara ya kwanza ulipomuona kibabu?”Binti: “mh….Pesa, eeh! Pesa. Suti aliyovaa, gari anayoendesha, vyote viliongesha kuwa ana pesa”Mhoji: “aah okay..!! Sasa ina maana hukujali vitu vingine?”Binti: “ mhh! Hapana. Umri, background yake, kazi yake, havinihusu. As long as ana pesa”Msimuliaji:Ah Binti akaweka pozi matata Kibabu akaona huu ni msosi akaja Binti akamkonyeza kibabu, kibabu akajibu Kibabu akafungua pochi binti akiifungua zipuBinti akavua nguo zake za mwili akideka Akimwacha yule kibabu tajiri akitweta Hakujali kuitwa malaya hakuona haya Kwa maana akili yake iliwaza pesaAkathibitisha kibabu ana sumni za kutupa Alikuwa na mvi kuonyesha umri pia ni mkubwa Akajisemea “kibabu anafaa kuwa baba yangu Ni ajabu kuona anapiga tour kwa machangu”Akaendelea kuwaza “labda pengine hana mke Kwamba ndo’ maana huu utamu anaufata nje? Au mkewe ni mvivu utamu anaupata nusu?” Akaacha kuwaza baada ya kugundua hayamuhusuBinti akalikabidhi tunda Ilikuwa shughuli kamili shahidi kuta Alijituma kuigiza furaha ilipobidi Aishinde dhiki maana babu alimuahidi bundaBinti akaweka mashauzi ki-star mpaka Kibabu akaenda round kadhaa hata Vyumba vya jirani wote walishtuka Kumsikiliza babu anatoa sauti za raha ah!Na sisi mashahidi tulikuwepo Na hii ndio inafanya hii hadithi iwe special Binti aliwaza leo, hakuikumbuka jana na upeo wake Haukumruhusu kuitabiri keshoMhoji: “aah okay kibabu”Kibabu: “mh ndiyo”Mhoji: “Kwanza naruhusiwa kukuita kibabu? Maana najua hilo sio jina lako halisi”Kibabu: “ heh! He heee! Aah Hapana shida, hapana shida nimekuwa nikiitwa hilo jina kwa muda mrefu na vijana wananitania…kwahiyo hakuna shida unaweza tu ukaniita kibabu”Mhoji: “Mh okay basi nitakuita kibabu na nilitaka kujua ni kawaida yako kuwa unanunua hawa madada wanaojiuza au ni mpenzi wa kutembelea haya maeneo mara kwa mara?”Kibabu: “mmmh! Kwakweli siwezi kusema ni tabia yangu, mhh hapana, japo nimefanya mara mbili mara tatu. Siwezi kusema nafanya ninafanya hivyo mara kwa mara kwamba ni tabia yangu lakini ni….Ukishaoa utajua kwamba kuna muda ndoa ina changamoto za hapa na pale…alafu uta.. unafahamu wewe ni mwanaume”Msimuliaji:Ah! Kibabu akaliona pozi matata Kwakuwa ana noti hakuona ugomvi kumfata Kibabu akakonyezwa kibabu akaji Akaifungua pochi kuona binti akiifungua zipuKibabu alitokwa na mate Hata noti zilizomtoka si chache Hakufikiri ada za watoto za masomo Alisahau yote kwa maana ubongo uliwaza ngonoAkamtazama yule binti maridadi Akajiuliza “vipi kaichagua hii kazi” Na umri wake ni mdogo anaweza kuwa binti yangu Ni ajabu kuona ngono anashiriki na vibabu” ah“Ah au labda ameondokewa na wazazi! Au wapo ila amelelewa kijambazi Au hali ngumu au usawa hauruhusu?” Akaacha kuwaza baada ya kugundua hayamuhusuKibabu akaonyeshwa njia ya mwezini Akampamba binti pesa ka’ Malkia enzini Alikuwa ka’ karogwa raha zilimzonga bila Uwoga akajitosa kuingia penziniAh na sisi tuliosimuliwa tuliokuwepo Ndio inayofanya hii hadithi iwe special Babu aliwaza leo hakuikumbuka jana na Umri wake ulifanya asitake kuiwaza kesho Ah!Mhoji: “Mh!!! Mhu! Okay!? Okay!! Okay!! Mmh mnaniacha njiapanda!! Eeh… Na hivi ni lini hasa mlikuja kugundua kuwa ninyi ni mtu na binti yake!??”Binti: …… Kibabu: ……

More From This Album

More songs from this album

Join The Family

New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.

© 2026 Panorama Authentik. All Rights Reserved.