LYRICS

Search for a song or choose an album and track.

THE VERTELLER album cover

THE VERTELLER

Dizasta Vina

Muscular Feminist

THE VERTELLER • Dizasta Vina
Lyrics copied!
Dear boys dear… menNi sisi wasichana kina dada, mabinti na mama zenu Tunaongea kutoka upande wa chini, upande mbali upande kutoka usawa wenuUpande nilipo msichana kuna hitilafu ‘So’ sikio lako thabiti ni ushindi kwangu Ninayotaka kusema hapa sio siri katu Ili ujue nina vingi vya ku-offer kabla ya mwili wanguKwa miaka mingi nimeishi gizani Gizani kwenye baridi na miba mingi nyikani Eneo uliotaka niishi ni eneo kandamizi Na bahati mbaya we’ ndo’ mchoraji wa hii ramaniRamani inamwonyesha binti kama chombo cha mapenzi Msindikizaji mtoto tegemezi Ramani isiyojua vituo Isiyojua tunaweza kuwa marafiki bila kuvuana nguoDear boys, dear menMngeelewa mngeiweka fikra sahihi Kama sanaa jinsi inavyozalisha fasihi Mi’ ni mlezi ukinivika mi’ umeivika jamiiU-gentlemen sio kulipa mgahawani Umeshapitwa na wakati Hainisaidii kunifungulia mlango nikifika kwenye gari Nifungulie fikra nitafakariDear boys, dear menTumekuwa tegemezi maana mmeficha mbegu Nani wa kuipigana vita yetu Umbali kati yetu utakuwa mkubwa milele Maana si ni wahanga wa mifumo mliyoiunda wenyeweNikijaribu kusoma nabaki bure Maana unajali mwili wangu, ndo’ maana sitaki shule Kila nikienda popote wanaomba ngono Labda niwe changudoa to the fullest At least I’ll get paidHata sisi tuna life too And the world doesn’t revolve around you Nipo tofauti sikupenda, na tena Unaponichezea fahamu kuwa ninazeeka mapemaShujaa unakumbukwa mzazi sikumbukwi Na kwanini kuwa msafi sio haja kwako Au kutembea kifua wazi ni kujiamini Nikitembea mimi ni nusu uchiI wish ungejua pride yako nayo sumu I wish ungejua kuwa uanaume sio nguvu I wish ungejua kuwa binadamu hajakamilika Mwanaume aliyekamilika anatimiza majukumuI wish ungejua kuwa na mimba sio haya I wish ungejua mwanamke kuwa kichwa si vibaya I wish ungejua kuwa upendo nao una nguvu kwahiyo mwanamke akitongoza mwanaume si malayaI wish ungejua kuonyesha fear sometimes, it’s okay It’s okay kulia sometimes I wish ungejua uongozi hauoni jinsia si Tatizo mwanamke kuongoza njia sometimesMifumo mliyoianzisha ina maisha Na chenye maisha kinazikwa Kwahiyo ipo siku mwanamke atasimama Na vita tunayopigana tutashindaInasikitisha hamkui kihisia, japo mnakua kiakili Natamani … natamani mngejua kuwa inauma sana kuwa namba mbili kwenye kila nyanjaEgo ni power ila iogope Maana ni upanga unaokata pande zote Ngoma nzuri ngoma nzuri haitavuma milele Ukitumia ubabe vibaya utakuvunja mwenyeweHadithi ya mwanamke alimshawishi Adam kula tunda Iliandikwa na wewe Sijui Delilah alichukua nguvu za mumewe akaziuza Iliandikwa na weweUpande wangu wa hadithi haujasikilizwa Pengine hautasikilizwa hasirani Maana ulianzisha shule akasoma mwanaume Mwanamke nikabaki nyumbaniDear boys, dear menHamtakaa kwenye kilele Maana kilele ni kuwa mama Mi’ ni kichwa sio wewe ungekuwa kichwa Mtaani kusingekuwa na single mothersLini mtaacha kutuita mademu Au labda mwite demu mama’ako Ukiona hauwezi naomba niheshimu kwa maana heshima inaanza kwakoNa haja ya maelewano iko hapo I mean… ipi salama ya kichwa cha familia bila Mkono wa kuosha macho?Najua tupo tofauti Na tofauti yetu itabaki, itabakia hivyo milele Ila naomba usinichukie nieleweDear boys, dear menNi sisi wasichana, kina dada, mabinti na mama zenu Tunawasilisha kutoka upande wa chini upande wa pili Upande mbali kutoka usawa wenuDear girls, dear WomenNi sisi kina kaka, kina baba, wanaume machizi wenu Tunaongea kutoka upande wa juu, upande wa mbali Upande uliowekwa na asili yetuUpande wenye mafungu yenye ulanguzi Upande wenye uthubutu na maamuzi Upande wenye machozi jasho na damu Uongozi upako ufahamu, upande usio na uhuru na uchaguziUpande uliofanya wanaume tutengwe na tunu Tutengwe na tunu Upande ambao pengine kuishi wewe ni ngumu Upande ambao asali yake ni kilele cha sumuUpande ambao haushabikii tija ya upendo au furaha au amani Kama hauangalii pima utagundua upande niliosimama mimi ni ngao ya jamii nzimaUanaume sio ushindi ni jukumu Uanaume sio rizki ni hukumu Ungejua kwanini wanaume wana msongo wa mawazo pengine ungefurahia udogo wakoDear women , dear girlsMmekuwa chombo cha ngono Maana mmetufanya chombo cha fedha Kama nguo hazitabadili mishono Hatuwezi kuwa marafiki bila ngono nawaelezaMnapoona padogo pana taswira ndefu Kiasi haujui si ndio tuliopigana vita yenu Hata mkiamka mmekuwa wanaume leo Mtagundua kuwa jinsia sio cheoWapendwa tukishindana mtashindwa Hata mkishinda ushindi wenu hautalindwa Kama ambavyo kila mmoja anatumia choo chake Kila mmoja a-play role yake na awe bingwaDear womenNdoa sio mafanikio Kuna wengi wanakonda maana ndoa zao sio Ndoa ni mwiba usijivune Ukiipata niamini unaweza kukamilika bila mumeDada baki shule bila elimu utateseka Ukitegemea urembo ipo siku utazeeka Kama ukiweka mwili wako hisani Ukizeeka tutajali ulichonacho kichwani‘Skiza’ hata wanaume tuna doubts too And this world doesn’t revolve around you Tuna stress zinatufunga na tena Kazi zetu ni ngumu ndo’ maana tunakufa mapemaKama unahisi upo huru umepotoka Hauwezi kuwa huru wakati umelipiwa posaDear womenIt’s okay kuwa namba mbili Majukumu sio mashindano acha kukaliliIt’s okay kumlea mwanaume asiye na kazi Ukaendelea kumuheshimu bila kumshusha hadhi Mbona sisi tunalea wanawake masikini wamekata ringi na bado mtaani hatutatangaziMwanaume ana jukumu la kujenga msingi? No, msingi unajengwa na elimu Kwa mfano nani anayekubali kucheza uchi kwenye videos? Jiheshimu nikuheshimuUrembo pia ni power, ila ni power na iogope Maana ni upanga unaokata pande zote Ngoma ya uzuri haitovuma milele Ukiutumia urembo vibaya utakuvunja mwenyeweI wish ungejua unachowaza ni muhimu Ukifanyia kazi na kuwa wa kwanza si’ majibu I wish ungejua kwamba asili imenipa umwamba Nikulee, kukulea wewe ni msaada si’ wajibuI wish ungejua tuko tofauti hata utunge dini Hauwi mwamba kwa kumweka mwanaume chini I wish ungejua kuwa kichwa ni hukumu Maana hakuna kinachotisha kama jukumuWangapi tumelelewa na hao single mothers Maskini and we turned out just fine Maybe idea ya kuacha kujali mtoto sababu Baba mjinga ingeachwa far behindTunasubiria uhalisi ubadilike Labda uhalisia haubadiliki huu Labda ni wakati wa kukubali ili yaishe kwamba Mtoto ni wa mama na baba ni rafiki tuLini mtaacha kutuita madanga ma-sponsors? Ndio, niheshimu nikuheshimu nitaacha wewe Ukiona imetosha, au sio?Najua tuko tofauti Na tofauti itabaki hivyo milele Usinichukie nieleweDear girls, dear womenNi sisi kina kaka kina baba, wanaume machizi wenu Tunawasilisha kutoka upande wa juu, upande mbali uliowekwa na asili yetu

More From This Album

More songs from this album

Join The Family

New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.

© 2026 Panorama Authentik. All Rights Reserved.