LYRICS

Search for a song or choose an album and track.

THE VERTELLER album cover

THE VERTELLER

Dizasta Vina

Ndoano

THE VERTELLER • Dizasta Vina
Lyrics copied!
Okay Ah Chukua kitabu fungua page sixty three Tusome hii part ya love and its mystery Haiwezi elezwa kwa science, math labda history Inaitwa ndoa ni half loss half victoryKauli ya kwamba sikuachi mpaka kifo ni kama sifa Inasemwa na wengi ila wachache wanamaanisha Wale wapambe na mashahidi wa kujivika Au keki na maua ambayo mwisho hupukutika ni....Nini maana ya suti shela au rangi ya bazee? Nini maana ya vile vikao kadi tarehe? Nini maana ya maandalizi hadi sherehe? Nini maana ya kiapo kwa padri na sheikh?Imeandikwa"kila penye watu lipo la kujifunza" Tembea uone kukaa ndani ni kujifunga Kama wanandoa si binadamu wanaofugwa Kwanini iwekwe ahadi isiyoweza kutunzwa? Ndoa ni.......?(mchagizaji) NDOANONdoa ni ile iliyoandikwa na sheria au dini? Au shuruti baada ya hatia ya kuzini? Ni jukumu unalovishwa baada ya ugoni? Au bashasha unalojivika usoniWatu wajue umeridhia, makubaliano na riba za njaa Ahadi ya kuwa pamoja kwenye shida na raha Ahadi inayovunjwa ka' sheria inavyopindwa na jamaa Ndoa si akiba ni sanaa Ndoa ni.....Sanaa ya kukaa nafasi ya mwenzi Sanaa ya kusahau maudhi na kuzikumbuka tenzi Za msamaha au kuzuga kujutia kitendo Sanaa ya kuzuga kubadili mwenendo Ndoa ni......Ule umoja mfano wa timu Kwenye mechi wanaomba mapumziko Ndoa inafungwa na sala na toba za mizimu Lakini inavunjika kwa meseji moja tu ya simu Ndoa ni......Hakuna kitu halisi kwenye ndoa labda huyo mtoto Ni idadi ya vipande baada ya kuvunja vyombo Ndoa si pete zinazozonga mikono Ndoa ni upendo unaobakia baada ya kuchoka kingono Ndoa ni...Ni ka' kikundi cha masela Wanaodhani kuwa wamekua Ndoa ni kuvumilia maudhi yanayokera Ndoa ni maigizo yasiyo na hela ndoa ni jela Ndoa ni....Kuzijua kelele Kutambua shangwe na vigeregere Ambacho hautajua milele Unapodondosha chozi kwa mchezo uliouchagua mwenyeweNdoa si.....kwa ajili yako ni kwa ajili ya watoto Kuweka ndoto kando na kuzivaa changamoto Ndoa ni kukumbatia kaa la moto Ndoa ni jua kali ndoa ni joto Ndoa ni....(mchagizaji) NDOANOAh Asiyejua ni nani? Kuwa mlioana msikitini na mkaachana mahakamani Kwa kuwa ndoa si nyepesi ndoa ni yai Ndoa ni kama kesi ya jinai, ndoa ni...Ndoa ni hukumu wanasema Ndoa ni ngumu jamani, ndoa ni sumu Au mpaka mume alete....UKIMWI nyumbani Ndio uamini kuwa ndoa si tunuNdoa ni maisha baada ya harusi Ile sherehe uliyoiota ndotoni Ndoa si drama mbele ya watu nyomi Ndoa ya kweli huanzia moyoniNdoa ni....FUMBO

More From This Album

More songs from this album

Join The Family

New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.

© 2026 Dizasta Vina. All Rights Reserved.