–
LYRICS
–
Search for a song or choose an album and track.

THE VERTELLER
Dizasta Vina
The Verteller Intro
THE VERTELLER • Dizasta Vina
Lyrics copied!
Inafaa kunena
Inafaa kunena labda ni muhimu sijui
Labda kusimulia si karama kama wanavyosema
Ikiwa msimuliaji huingia hatarini
Labda kweli baraka ni laana njemaWasikilizaji nasikia wana ndoto na wenyewe
Si uongo
Hadithi nzuri ndo' kilele kwa wasikilizaji
Ila ndoto ya msimuliaji
Ndoto ya msimuliaji ni kulindwa milele
Kwanini azibwe mdomo wakati ubongo unapiga kelele?Si lazima msimuliaji apazwe la hasha!
Atandikiwe majani au aandikwe kama mwanasiasa
Lakini lengo lake awe huru msimuliaji atambe
Alindwe ili waovu waonyeswe, mashujaa watangazweOna kuna wasimuliaji hukwepa pande tupu
Yani baada ya mitaji husimulia upande wa wenye nguvu
Wapo wabinafsi wanaotangaza jinsi asili ilivyowahusudu
Husimulia walivyoshinda vita wakigombea asali na waduduSwali ni je? , Nani atasimulia hadithi ya wadudu?
Nani atasimulia kua si mara zote mchukua asali alimsulubu mdudu?
Nani atasimulia hadithi ya shetani, baada ya kusikia upande wa Mungu?
Baada ya kusikia upande wa MunguWaungwana kumbukeni ya muhimu na ziada
Kumbukeni ya uchumi jamii na siasa
Lindeni ghala la chakula na maji
Lakini msisahau kumlinda msimuliaji, ni afyaJapo kuwa msimuliaji si alama ya taifa
Lakini fikiria mtu ambaye yupo tayari kulipa gharama ya maisha
Msimuliaji hukukumbusha ulipotoka ujuе unapoenda
Na hiyo ndio faidaLabda ukumbuke ya mdimu na majoka
Au simulizi za mizimu ya mloka
Au tarihi ambazo ni historia za kuziheshimu
Maana asiyеijua historia, huweza kurudia makosaMsimuliaji hachagui upande maana hapendi kupotoka
Hafungamani na misalaba au alama za mwezi na nyota
Alama za wasimuliaji walioidongosha kheri
Waliookota sifa wakati wakiidondosha kweli
Wakati wakiidondosha kweliEnyi wa khaki kijani na manjano
Mmeona nyekundu ile pale?
Haijaja pale leo ipo tangu kale
Msiruhusu iwaguse
Si kwakua hamna hadhi
La hasha
Ila ile rangi anaifahamu msimuliaji
Ile rangi ni damu iliyomtoka au kumrukia
Na mchanganyiko wa pande zote za dunia
Anaijua leo, aliijua jana
Hajaisoma au kuisikia
Aliipata wakati akitafuta vya kusimulia
Na ni hivi anavyotaka kukusimulia leoNyakati za katikati kwenye eneo la ukanda wa kidachi
Zilizaliwa lugha tatu, Lugha ghafi
Na kati yao ilikuwepo lugha iliyoitwa lugha ya watu
Kwenye ukanda huu msimuliaji hakuitwa Narrator au story teller kwa kiingereza
Hakuitwa Erzahler japo kuwa ukanda huu ulikuwa karibu sana na Ujerumani
Hakuitwa Rawi kwakua huu ukanda haukuwa wa kiarabu
Msimuliaji aliitwa the VertellerKama Christopher Hitchens
Ama Professor Laurence Krauss
Ama Shaaban Robert
Ama Francis Scott Key Fitzgerald
Ama Chimamanda Ngozi
Ama Fred Saganda
Ama Alice Walker
Ama Octavia Burtler
Ama Lufufu Mkandala
Ama Rainfred Masako
Dizasta vina, mabibi na mabwana
Ni the Verteller
More From This Album
More songs from this album
Join The Family
New music. Stories. Early access. Things you won't find everywhere else.
© 2026 Panorama Authentik. All Rights Reserved.